WAZIRI ZUNGU AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA HONG YU STEEL COMPANY LIMITED KILICHOPO KIBAHA -PWANI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na MazingiraMhe. Mussa Azzan Zungu amefaya ziara katika kiwanda cha Hong Yu steel Company Limited kilichopo kata ya Zegereni wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani, ili kujionea uzalishaji wa kiwanda hicho kama kinafanya uzalishaji wake kwa kuzingatia sheria na kanuni za Maazingira.
Kiwanda hiki kinazalisha nondo kwa kutumia malighafi ya vyuma chakavu kutoka kwa wakusanyaji mbalimbali Nchini.
Katika ziara hiyo Mhe. Zungu aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Prof. Esnat Chaggu, Meneja wa kanda ya Mashariki Bw. Arnold Mapinduzipamoja na kikosi kazi cha NEMC.
Mhe. Zungu ameeleza kuwa katika uendeshaji wa shughuli hizi kunautaratibu wake endapo kutabaini kunamakosa yanafanyika ambayo yanaenda kiyume na sheria hatua za kisheria zitachukuliwa.
Pamoja na changamoto zinazowakabili wawekezaji wengi hapa nchini kwa upande wa upatikaji wa malighafi ya chuma serikali bado inashughulikia tatizo hili “Ni kweli Nchi inauhaba wa malighafi hizi lakini isitumike kuwa ndio sababu ya uharibifu wa miundombinu ya Serikali miundombinu yote ya serikali ambayo itaharibiwa wale wote watakao husika hatua za kisheria zitachukuliwa.”alisema Mhe. Zungu
Aidha Mhe. Zungu amemuagiza meneja wa NEMC Kanda ya mashariki Bw. Mapinduzi kwa kushirikiana na mamlaka ya ulinzi na Usalama pamoja na mamlaka ya Reli kuhakiki malighafi inayotumiwa na kiwanda hicho.
“kwa mujibu wa taarifa tulizopata kutoka kwa wahusika chuma hiki kinatoka china, lakini wataalam wetu wanauwezo wa kujua kama vyuma hivi ni mali ya Serikali. Hivyo nimemuagiza meneja wa kanda ya mashariki wa NEMC kwa kushirikiaa na mamlaka ya ulizi na usalama pamoja na mamlaka ya Reli kukagua vyuma hivyo na kujiridhisha”.
Kwa upande wake Bw. Arnold Mapinduzi Meneja wa Kanda ya Mashariki (NEMC) ameeleza kuwa “Mhe. Waziri alipata taarifa kuwa kunavyuma chakavu vinashushwa katika kiwanda hiki, kikosi kazi cha NEMCwamebaini hayo magari yanavibali vyote isipokuwa kiwanda hakikuwa na kumbukumbu ya nyaraka za kufuatilia mzigo (tracking document), inawezesha Serikali kufuatilia mzigo unapofikia .”
Aidha Mhe. Zungu pia alitembelea kituo cha polisi cha Oysterbay kujionea vyuma chakavu vilivyosafirishwakutoka mbeya kuelekea Dar es Salaam bila kibali na kubaini walikuwa wanatumia kibali cha mtu mwingine ambacho kimeshapita muda wake.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15