NEMC NA TAWA WAADHIMISHA SIKU YA KOBE HIFADHI YA ZOO TABORA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya wanyamapori (TAWA) wameadhimisha siku ya Kobe Duniani leo tarehe 23, Mei kwakutembelea bustani ya wanyama ya Tabora Zoo yenye Kobe takribani miambili (200) na kutoa elimu ya uhifadhi wake kwa wanafunzi na jamii inayowazunguka.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea eneo la hifadhi ya Kobe Kaimu Meneja NEMC Kanda ya Kati Bw. Novatus Mushi amesema Baraza kwa kushirikiana na TAWA limetumia siku ya leo kuelimisha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa maisha ya Kobe Duniani na kueleza fursa za kimazingira zilizopo katika kuwatunza.
Ameongeza kuwa ni muhimu kuepukashughuli za kibinadamu kama vile kuchoma misitu na uchafuzi unaotokana na plastiki kwani zimekuwa zikiathiri mifumo ikolojia ya Kobe na hivyo kuhatarisha uwepo na ustawi wake.
Kwa upande wake msimamizi wa bustani ya wanyama pori ya Tabora (Tabora Zoo) Bw. Abubakari Shaban amesema Kobe ni nyara ya Serikali na ni kosa kisheria kumiliki Kobe bila kibali kutoka Mamlaka ya TAWA na kuwasisitiza wananchi kuwa wanapowakuta Kobe katika maeneo yasiyo rasmi waijulishe TAWA ili iwapeleke katika maeneo salama.
Baraza linaendelea kusisitiza kwa kilamwananchi aepuke shughuli zozote zinazoharibu Mazingira na makazi ya wanyama kwa ujumla ili kutunza Mazingira kwa manufaa ya viumbe vyote wakiwemo Kobe pamoja na kuendelea kuvutia utalii katika nchi yetu.
Ziara hiyo ilihusisha wanafunziwa shule ya Sekondari Kaze Hill pamoja na majirani wanaoishi karibu na bustani hiyo ya wanyama pori.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15