Kurugenzi ya Tathimini ya Mazingira (DESIA)
Kurugenzi inaongozwa na Mkurugenzi
Lengo
Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya tathmini ya athari za kimazingira na kijamii za miradi mipya na iliyopo.
MAJUKUMU
- Kusimamia mchakato wa usajili, na udhibiti wa tathmini ya athari kwa mazingira
- Kujenga uwezo wa Wizara za kisekta na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika tathmini ya athari za kimazingira na kijamii
- Kupitia na kuandaa miongozo na taratibu za kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Kijamii (ESIA) na Ukaguzi na kusambaza kwa wadau.
- Kusimamia na kuratibu uchunguzi na uhakiki wa muhtasari wa mradi, ripoti za upeo na kuidhinisha hadidu Rejea za kufanya tafiti za ESIA na Ukaguzi wa Mazingira (EA).
- Kuratibu mapitio ya ripoti za ESIA/EA na mikutano ya Kamati ya Ushauri ya Kiufundi ili kujadili ripoti zilizowasilishwa.
- Kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohusiana na mapitio ya ripoti za ESIA/EA
- Kuwezesha mchakato wa utoaji wa Vibali vya Muda kwa miradi inayohusiana na Viwanda
- Kuratibu Mamlaka za Wilaya, Wizara za Kisekta na ushiriki wa Umma katika mchakato wa mapitio ya ESIA.
Habari na Matukio
Matukio
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15