Kanda ya Kaskazini
Ofisi ilipo
Ofisi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kaskazini iko Arusha, kwenye makutano ya Barabara za Makongoro – Goliondoi, mzunguko wa Ngorongoro, Kitalu Na. 055019 /1 & 055019/6, Jengo la Kituo cha Utalii cha Ngorongoro, Ghorofa ya Sita. Kwa hiyo, unaweza kuwasiliana na Ofisi kwa anuani ifuatayo:
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) – Kanda ya Kaskazini,
Makutano ya Barabara za Makongoro – Goliondoi,
Kitalu Na. 055019 /1 & 055019/6,
Jengo la Kituo cha Utalii cha Ngorongoro,
Ghorofa ya Sita,
S.L.P. 1041,
Arusha,
TANZANIA.
Simu: +255 738 064 966
Barua pepe: nemcarusha@nemc.or.tz
Ofisi ya Kanda ya NEMC ilifunguliwa mwaka 2005, baada ya kumalizika kwa mradi wa UNDP/GEF East Africa Cross-Border Biodiversity Project (1999-2004) ambao kwa upande wa Tanzania ulikuwa unatekelezwa na NEMC, na Ofisi yake ilikuwa Arusha. Hivyo basi, Ofisi hii ilikuwa ya kwanza kuanzishwa kati ya Ofisi za Kanda za NEMC, ikiwa na lengo la kusogeza huduma karibu na wadau.
Majukumu
Ofisi ya Kanda inamwakilisha Mkurugenzi Mkuu katika kutekeleza Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 (Sura 191), na majukumu yake ni pamoja na: Kukuza Uelewa kuhusu Mazingira kwa wadau; Kupanga mipango na kufanya Tafiti za Mazingira; Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira; Tathmini ya Athari kwa Mazingira; Upelembaji wa Mazingira; Uratibu wa shughuli za Mazingira; na shughuli zingine ambazo Baraza linatakiwa na Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kufanya.
Eneo la Kazi
Kanda ya Kaskazini inajumuisha Mikoa mitatu ambayo ni Arusha, Kilimanjaro na Manyara, na ina jumla ya eneo la Kilomita za mraba 95,348 km2, ambalo kulingana na Sensa ya mwaka 2012 lina jumla ya watu 4,759,528. Mikoa hii mitatu ina Wilaya kama inavyooneshwa hapa chini:
- Arusha - Arusha, Meru, Longido, Monduli, Ngorongoro, na Karatu.
- Kilimanjaro - Same, Rombo, Mwanga, Moshi, Hai na Siha.
- Manyara - Babati, Hanang, Mbulu, Simanjiro na Kiteto.
Mipaka
Kwa upande wa Kusini, Kanda hii inapakana na Mikoa ya Singida, Dodoma na Morogoro; Upande wa Kaskazini inapakana na Kenya; Upande wa Magharibi Mikoa ya Simiyu na Mara; Upande wa Mashariki inapakana na Mkoa wa Tanga
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15