Maswali

Bidhaa ambazo hazitaathiriwa na katazo hili ni pamoja na vifungashio vya bidhaa kama vile vifungashio vya madawa, vifungashio vya vyakula kama vile: maziwa, korosho, n.k bidhaa za viwandani, kilimo na ujenzi. Hata hivyo, vifungashio ni lazima vikidhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Vifungashio hivi haviruhusiwi kutumika kama vibebeo.

Serikali imeamuakupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki ili kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo. Athari za mifuko ya plastiki ni pamoja na kutooza katika mazingira kwani inakadiriwa kudumu hadi zaidi ya miaka 500 na hivyo kuleta athari za muda mrefu; uchafuzi wa mazingira hasa kwa mifuko hii kuzagaa ovyo katika mazingira; kuziba miundombinu ya majitaka na mifereji ya mvua na kusababisha mafuriko; kuharibu mfumo wa ikolojia na bioanuai, vifo vya mifugo na wanyama wengine hususan mifugo na viumbe wa baharini wanapokula na kumeza mifuko hii.

Katazo hili linaanza tarehe 1 Juni,2019.

Katazo hili linahusu kupiga marufuku uzalishaji, uingizaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya plastiki vibebeo vya aina zote(carrier bags).

Waweza kuwasilisha malalamiko yako NEMC kupitia Simu ya kiganjani namba 0692108566 , Barua pepe dg@nemc.or.tz, Sehemu ya malalamiko iliyopo kwenye tovuti ya NEMC, kutembelea ofisi za Baraza zilizopo karibu, barua, n.k