Elimu ya mazingira

NEMC hutoa elimu ya Mazingira kwa Umma kwa kujenga uelewa kupitia vyombo vya habari, majarida, mikutano, semina na mafunzo mbalimbali kuhusiana na utunzaji na uhifadhi wa mazingira pamoja na kuelewesha kwa upana umuhimu wa kutunza mazingira katika jamii.