BODI YA NEMC AWAMU YA TISA YAZINDULIWA RASMI, YAAHIDI KUFANIKISHA MCHAKATO WA NEMC KUWA MAMLAKA

Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) awamu ya tisa, chini ya Mwenyekiti wake Bi. Mwanasha Rajab Tumbo imezinduliwa rasmi na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Yusuf Masauni leo tarehe 15 Aprili, 2025 katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma.
Akizindua Bodi hiyo yenye wajumbe nane Mhe.Masauni amesema ni kufuatia uteuzi uliofanywatarehe 9 Aprili, 2025 ambapo watatumikia nafasi walizopewa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mhe.Masauni amesema Bodi hii imekuja wakati Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) liko katika mchakato wa kuwa Mamlaka ambapo mchakato wake upo katika hatua nzuri.
"Mchakato wa kuifanya NEMC kuwa Mamlaka usingeweza kufanikiwa katika bunge lililopita kwa sababu ya mlolongo wake, lakini kwa sasa upo katika hatua nzuri na tunaamini Bodi hii itakuwa msaada mkubwa katika kufanikisha hili" Amesema Mhe. Waziri Masauni.
Akijibu hoja ya Mkurugenzi Mkuu (NEMC) Dkt. Immaculate Sware Semesi ya kukosekana kwaMamlaka yenye nguvu ya kusimamia na kudhibiti changamoto za Mazingira, Mhe. Waziri amesema kwa sasa kipaumbele cha utekelezaji ni kuifanya NEMC kuwa Mamlaka ili iongeze makali katika kutatua changamoto za Mazingira.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Cyprian Luhemeja amesema Tanzania inabadilika na inahamia kwenye Mazingira na katika Sheria ya Mazingira sura namba 1991 inaitambua NEMC kama chombo chenye dhamana ya kusimamia Mazingira hivyo ameutaka Uongozi kuipa NEMC Mamlaka itakayoweza kushughulikia mahitaji ya sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo Bi. Mwanasha Rajab Tumbo alipozungumza amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo naameahidi kuisimamia NEMC katika kutekeleza majukumu yake na kuwataka watumishi wote kuwa na ushirikiano ili kufanikisha mipango yote.
Wajumbe wanaounda Bodi hiyo ni Bi. Kemilembe Salome Mutasa, Dkt. Abubakar Salum Rajab, Prof. Hamis Masanja Malebo, Prof. Theobald Frank Theodory, Mha. Bashir Jums Mrindoko, Bw. Said Habibu Tunda, Bw. Alex Mgongolwa na Bi. Rabia Abdalla Hamid.
Uteuzi wa Bodi hii umekuja mara baada ya bodi iliyopita kumaliza muda wake.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15