NEMC yataka taasisi zishirikiane kuratibu uchimbaji mchanga katika mito


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC)limependekeza NEMC, Hamashauri za Wilaya, Wasimamizi wa Mabonde na Kamisheni ya Madini kushirikana kuandaa mwongozo wa uchimbaji endelevu wa mchanga katika mito ya Tanzania.

Pendekezo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka alipotembeleaeneo la Matosa, Wilaya ya Ubungo unakopitaMto Mbezi. Ziara hiyo imesaidia watumishi wa NEMCkujionea mwenyewe hali ya mazingira na madaraja ilivyo kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Dk Gwama amewahamasisha vijana wanaochimba mchanga kujiunga katika vikundi ili wapewe utaratibu wa kufanya shughuli ya uchimbaji mchanga endelevu.

“Tukiweka utaratibu wa pamoja tutaweza kutengeneza ajira kwa vijana na pia halmashauri zutakusanya mapato,” amesema Dk Gwamaka na kuongeza kwamba mazingira yatatunzwa iwapo utakuwepo utaratibu unaofanya uchimbaji wa mchanga kuwa endelevu.

“Tayari Mkuu wa Mkoa ametoa waraka kwa halmashauri zote kushirikiana na NEMC na Wizara ya Madini kuandaa mpango endelevu wa uchimbaji wa mchanga katika mito ya mkoa wa Dar es Salaam,” amesema Dk.Gwamaka

Ameeleza kuwa mito hujaa maji kunatokana na uchafu na mchanga kuziba njia za mito na kisha kusababisha miundombinu kuharibika, na kuongeza kwamba uchimbaji mchanga ukiratibiwauharibufu wa miundombinu na mafuriko vitapungua.

“Ni muhimu kulinda miundombinu ya serikali ambayo inagharimu kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi. Hivyo lazima kuwe na utaratibu utakaofanya vijana kuchimba mchanga kwa namna endelevu,” amesema Dk Gwamaka

Amewataka vijana kuunda vikundi ili watambuliwe na serikali za mitaa yao ili pindi mwongozo ukitoka wapatiwe vibali vya kufanya uchimbaji ulio endelevu na kuwapo urahisi wa kuwafuatilia.

“Hatua hii itapunguza gharama kwa serikali ya kufanya ukarabati wa miundombinu iliyoharibika,” amesema Dk.Gwamaka

Vijana wachimbaji wamueleza Dk Gwamaka kuwa kazi yao inasaidia kupunguza mafuriko kwa maelezo kwamba wakisafisha maeneo maji hupita kwa urahisi.Wamesema chagamoto yao kubwa ni vibali vya kufanya shughuli hiyo.

Bwana Jeremia Kitomali ameiomba Serikali kutoa vibali vya kuchimba mchanga katika mito na kueleza kwamba shughuli yao inasaidia kuondoa uchafu kwenye mito na kurudisha kina cha mto katika hali yake halisi.

“Licha ya kwamba tunapata kipato kupitia uchimbaji mchanga kwenye eneo hili nakulifanyia usafi, mara kwa mara tumekuwa tukikamatwa kwa kukosa kibali. Tunaomba mtusaidie,” amesema Bw.Kitomali

NEMC itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kushirikiana na wadau wake ili kuhakikisha mazingira yanalindwa na kuhifadhiwa ikiwa ni pamoja.Sasa hivi inapendeza uwepo mwongozo wa uchimbaji endelevu wa mchanga katika mito ili wachimbaji wanufaike na mazingira yalindwe.