NEMC YAENDESHA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MAMLAKA ZA SERIKALI KATIKA MIPAKA


NEMC YAENDESHA MAFUNZOKWA WATUMISHI WA MAMLAKA ZA SERIKALI KATIKA MIPAKA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeendesha mafunzo ya siku mbili yahusuyo Usimamizi na Ukaguzi wa bidhaa hatarishi kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali zilizopo Mipakani.

Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo wa namna sahihi ya kuenenda katika kuhakikisha Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake katika udhibiti wa taka hatarishi inazingatiwa hasa udhibiti wa uingizwaji na usafirishaji wa bidhaa hatarishi nchini kwa maslahi mapana ya mazingira.

Taasisi zilizoshiriki mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa St Gaspar Dodoma ni pamoja na TBS, Ofisi ya makamu wa Rais, TPHPA, TRA, GCLA pamoja na Kitengo cha Usalama wa Afya Mipakani.

Mada zilizofundishwa ni pamoja na :-

  • Uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria katika kudhibiti taka hatarishi
  • Mfumo wa Kisheria wa Udhibiti wa biashara ya mipakani ya bidhaa zenye athari kwa Mazingira
  • Mambo ya kimazingira ya kutilia maanani mipakani
  • Mfumo wa kisheria wa udhibiti wa biashara ya bidhaa ya plastiki mipakani pamoja na
  • Mradi wa majaribio wa kupunguza taka hatarishi