WAZIRI JAFO ASISITIZA UPANDAJI MITI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ameelekeza kila mwanafunzi apande mti, kuusimamia na kuutunza hatua itakayosaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Dkt. Jafo ametoa maelekezo alipokuwa jijini Tanga wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kuhamasisha shughuli mbalimbali za hifadhi na utunzaji wa mazingira.