β€‹ππ„πŒπ‚ π˜π€π‡π€πŒπ€π’πˆπ’π‡π€ π”π’π€π…πˆ 𝐖𝐀 πŒπ€π™πˆππ†πˆπ‘π€ π’π‡πˆπŒπŒπ”π“π€ πŸπŸŽπŸπŸ“ - πŒπŽπ‘πŽπ†πŽπ‘πŽ


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia wanamichezo wake wanaoshiriki mashindano ya SHIMMUTA 2025 mkoani Morogoro wakichagizwa na kauli mbiu yao isemayo "π‘΄π’Šπ’„π’‰π’†π’›π’ π’π’Š π‘¨π’‡π’šπ’‚, π‘΄π’‚π’›π’Šπ’π’ˆπ’Šπ’“π’‚ π’π’Š π‘Όπ’‰π’‚π’Š" wameshiriki zoezi la kufanya usafi kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro siku ya kufunga mashindano hayo Disemba 6, 2025.

Wanamichezo hao wamefanya usafi huo ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa usafi wa Mazingira kwa watumishi wanaoshiriki mashindano hayo pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Morogoro.

Imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa wanamichezo hao kuhamasisha usafi wa Mazingira kila mwaka kwenye mashindano ya SHIMMUTA huku wakienzi maono ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi kuhakikisha Mazingira yanakuwa safi na yanaendelea kulindwa nchi nzima.

NEMC imeshiriki mashindano hayo ya SHIMMUTA 2025 ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya ya watumishi lakini pia kutumia fursa hiyo katika kutoa elimu kwa watumishi na Wananchi mkoani Morogoro kuhusiana na masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.

Katika kuhakikisha elimu inafika kwa watu wa rika zote pia wanamichezo hao wametoa elimu ya Mazingira na kukabidhi vifaa vya kuzolea na kuhifadhia taka katika Shule ya Msingi Mwere ambapo wanamichezo hao walikuwa wanatumia viwanja vya shule hiyo kwa ajili ya mazoezi kipindi chote wakiwa kwenye mashindano hayo.

Mashindano ya SHIMMUTA 2025 yenye Kauli Mbiu isemayo "π‘Όπ’π’π’ˆπ’π’›π’Š π‘°π’Žπ’‚π’“π’‚ π’Œπ’˜π’‚ π‘΄π’Šπ’„π’‰π’†π’›π’ 𝑬𝒏𝒅𝒆𝒍𝒆𝒗𝒖: π‘΄π’Šπ’„π’‰π’†π’›π’ π’π’Š 𝑫𝒂𝒓𝒂𝒋𝒂 𝒍𝒂 π‘¨π’‡π’šπ’‚, π‘¨π’Žπ’‚π’π’Š, π‘Όπ’Žπ’π’‹π’‚, 𝒏𝒂 π‘΄π’”π’‰π’Šπ’Œπ’‚π’Žπ’‚π’π’ π’˜π’‚ π‘²π’Šπ’•π’‚π’Šπ’‡π’‚" yalianza rasmi Novemba 23, 2025 na kufungwa rasmi Disemba 6, 2025 kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima.