NEMC YAKUTANA NA TAASISI ZA SERIKALI KUWAJENGEA UELEWA KUHUSU UTEKELEZAJI WA SHERIA NA KANUNI ZINAZOHUSU KELELE


NEMC imekutana na Wizara na Taasisi za Serikali kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa sheria na kanuni zinazohusu udhibiti wa kelele na mitetemo. Wizara hizo ni Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Mkuuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Taasisi hizo ni Wakala wa Usajili (BRELA), Wakala wa Vipimo (WMA), Ofisi ya Hakimiliki (COSOTA), Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Shirika la Viwango (TBS) na Polisi.