NEMC YAHESHIMISHA TANZANIA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUONDOA TAKA DUNIANI

Ni kauli yake Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ) Mhe. Khamis Hamza Khamis (Mb) alipokuwa akihutubia watanzania kwenye kilele cha siku ya kuondoa taka duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kinachoenda na kaulimbiu isemayo "wezesha taka sifuri kwenye sekta ya nguo na mitindo"
Amesema NEMC imeonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuratibu siku hii muhimu ikiwa ni hatua katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan za utatuzi wa changamoto za kimazingira zinazosababishwa na utupaji holela wa taka na kupelekea magonjwa ya mlipuko na mafuriko.
"Amesema uzalishaji wa taka umekuwa changamoto kubwa duniani kote, hususani katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza n.k. Takwimu zinaonesha kuwa, takribani kiasi cha tani millioni 7 za taka ngumu huzalishwa hapa nchini kwa mwaka ambapo wastani wa asilimia 45 hadi 50 tu hukusanywa na kutupwa dampo. Aidha, asilimia 50 hadi 55 hubaki kwenye mazingira na kuzagaa kwenye mito na mifereji ya maji taka na mitaro ya maji ya mvua NEMC nendeni mkatambue viwanda vinavyochafua mazingira, vinavyotirirsha maji machafu, kama wapo hawa wachukuliwe hatua kwa sababu moja ya jukumu lenu NEMC ni kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira"
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Immaculate Sware Semesi alipozungumza amesema siku ya Kimataifa ya kuondoa taka Duniani ilianzishwa ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu athari za taka kwa mazingira na kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali.
Amesema siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Machi ili kuhamasisha Serikali, Sekta binafsi, na jamii kwa ujumla kubadili mifumo ya uzalishaji na matumizi ili kufikia uchumi wa mzunguko na mazingira safi kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Ameyataja malengo ya siku hii kuwa ni kuhimiza kupunguza uzalishaji wa taka (reduce), kutumia tena bidhaa (re-use), na kuchakata taka (recycle) yenye kuleta tija katika matumizi bora ya rasilimali zetu ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Maonesho haya yameambatana na kaulimbiu isemayo kuwezesha taka sifuri kwenye sekta ya nguo na mitindo ilihali Kitaifa siku hii imebeba kaulimbiu ya TAKA NI FURSA.
Maadhimisho haya yaliyoshirikisha wadau wa mazingira na kuhudhuriwa na viongozi pamoja na wananchi yamepambwa na msanii nguli wa kughani vina na mizani wa bongo fleva Bw. mrisho Mpoto.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15