NEMC YAHAMASISHA USAFI WA MAZINGIRA KWA WANAMICHEZO - SHIMMUTA
Wanamichezo wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefanya usafi katika viwanja vya Usagara jijini Tanga mara baada ya ufunguzi wa Michezo ya SHIMMUTA leo Novemba 18,2024 yenye kauli mbiu isemayo "πΌππππππππππ: πΎππππππππππ π»ππππππππ πΌπππππππ ππ πΊπππππππ ππ π΄ππππ 2024 π²ππ πΌππππππ π©πππ ππ π΄ππππ ππππ ππ π»ππππ".
NEMC wamefanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza majukumu yake ya uhamasishaji wa kutunza Mazingira kama Taasisi pekee iliyopewa jukumu la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004.
Awali wakiwasili kwenye viwanja vya Usagara Wanamichezo hao wa NEMC walisambaza vifaa vya kuwekea taka kwenye viwanja hivyo pamoja na kuwakumbusha wanamichezo wengine umuhimu wa kutotupa taka hovyo na mara baada ya ufunguzi wakaingia uwanjani kuokota taka na kuweka kwenye vifaa hivyo vya kutunzia taka.
NEMC inashiriki mashindano ya Michezo ya SHIMMUTA inayofanyika jijini Tanga kuanzia Novemba 10 hadi 24,2024 ambayo yamefunguliwa rasmi Novemba 18,2024 na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Dotto Biteko kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15