​NEMC YADHIBITI SAUTI ZILIZOZIDI VIWANGO VIWANJA VYA SABASABA.


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limedhibiti sauti zilizozidi viwango kwa wadau, wafanyabiashara na watoa huduma wanaozalisha kelele chafuzi kwenye mabanda yao katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Udhibiti huo umefanyika kwa kutoa elimu ya madhara ya sauti zilizozidi viwango na namna ya kudhibiti, viwango vya decibel zinazotakiwa wakati wa mchana na usiku kwa maeneo husika, pamoja na umuhimu wa kuwa na kifaa cha kupimia sauti (decibel) ili kujua kama imezidi au la.

Mabanda ya maonesho yaliyotembelewa na kupewa elimu ya kudhibiti kelele chafuzi au sauti zilizozidi viwango uwanjani hapo ni pamoja na Vodacom, Tigo, Tantrade, Kijiji cha bima pamoja na Superdol.