NEMC, GCLA YAENDESHA MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA KEMIKALI KWA MAAFISA FORODHA MPAKA WA SIRARI.

Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Ofisi ya Madini waendesha mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali ya Zebaki kwa Maafisa wa Forodha kutoka mpaka wa Sirari na Maafisa Mazingira kutoka Wilaya zenye shughuli za uchimbaji wa dhahabu katika Hotel ya Victoria Palace iliyopo Jijini Mwanza.
Akifungua Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Huduma za udhibiti zikiwemo Kemikali kutoka Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw.Daniel Ndiyo amesema yamelenga kukumbushana wajibu uliopo kwa maafisa forodha na maafisa mazingira kwenye suala zima la usimamizi wa matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo.
Amesema Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuhakikisha madhara ya matumizi ya kemikali ya zebaki kwa wachimbaji yanadhibitiwa kwa kutekeleza matakwa ya Mkataba wa Minamata pamoja na kuwepo kwa Sheria zinazotoa miongozo ya utekelezaji wa matakwa ya mkataba huo ikiwemo Sheria ya Mazingira, Sheria ya Kemikali iliyopo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Kanuni mahususi za zebaki kwa ajili ya kutekeleza mkataba huo.
Ameongeza kuwa Maafisa Mazingira kwenye Wilaya husika ndio wenye wajibu wa kusimamia masuala ya mazingira katika maeneo yao, hasa maeneo ya uchimbaji hivyo mafunzo haya ni muhimu sana ili kuwajengea uwezo wa namna sahihi ya kuenenda katika kuhakikisha mazingira yanalindwa na kunakuwepo na matumizi salama ya zebaki kwa wachimbaji wadogo.
Naye Bi Amina Kibola Meneja wa maeneo Maalumu na Mabadiliko ya tabianchi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC alipozungumza amesema mradi huu kwa Tanzania unatekelezwa katika Mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Mbeya na Songwe huku ukiratibiwa na Baraza na jukumu la elimu kukasimiwa kwa ofisi ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Bi.Amina amesema malengo ya mradi huu ni kuimarisha taasisi husika kujenga uwezo na ujuzi katika kutekeleza matakwa ya Mkataba wa Minamata, kuwezesha mabadiliko ya Kisera, pamoja na kuboresha matumizi ya teknolojia
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15