​MRISHO MPOTO AZURU BANDA LA NEMC MAONESHO YA SABASABA


Msanii mashuhuri wa bongo fleva na mtaalam wa kutunga na kughani mashairi yenye vina na mizani Bw. Mrisho Mpoto azuru Banda la NEMC Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Alipozuru banda hilo alipokelewa na watumishi wa Baraza na kupatiwa elimu ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Kadhalika wananchi, wasanii, wadau wa mazingira, wizara, taasisi, vyuo, wafanyabiashara pia wamepata fursa ya kutembelea banda letu na kupatiwa elimu ya mazingira.

Elimu aliyopatiwa ni pamoja na umuhimu wa ulipaji wa ada ya Mazingira, madhara ya matumizi ya mifuko ya plastiki, udhibiti wa sauti zilizozidi viwango, matumizi salama ya zebaki kwa wachimbaji wadogo na uharibifu wa ardhi pamoja na umuhimu wa kufanya tathmini ya athari kwa Mazingira kabla ya kuanzishwa kwa mradi.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kupitia Banda lake lililopo Clinic ya biashara viwanja vya sabasaba limeendelea kutoa elimu ya uhifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa wananchi.

NEMC inawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda lake lililo jengo la Karume kupata ELIMU ya Mazingira msimu huu wa sabasaba.