​MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA KUANZA RASMI 29 /05/2024


Maadhimisho ya wiki ya Mazingira yenye kauli mbiu isemayo "urejeshwaji wa Ardhi, ustahimilivu wa hali ya Jangwa na ukame" yatakayofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma yatazinduliwa rasmi tarehe 29/05/2024 Mkoa wa Katavi kwa kufanya uzinduzi wa josho la mifugo na ugawaji wa hati miliki za kimila na hati za misitu 4450.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt.Seleman Jafo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa NEMC Jijini Dar es Salaam.

Amesema maonesho ya mwaka huu yenye lengo la kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa Mazingira yataambatana na matukio mbalimbali yakiwemo Uzinduzi wa mradi wa urejeshaji uoto wa asili unaotekelezwa Wilaya 7 katika Mikoa mitano nchini ambayo ni Iringa, Njombe, Rukwa, Mbeya na Katavi.

Kutafanyika pia uzinduzi wa kongamano la Mazingiar katika ukumbi wa JNICC Dar es Salaam tarehe 31 mei mwaka huu lenye kaulimbiu isemayo " Mabadiliko ya tabianchi na Mazingira ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdori Mpango.

Ameongeza kuwa tarehe 01/06/2024 ni siku ya kampeni ya usafi nchi nzima ambapo viongozi mbalimbali watakuwepo wakiongoza zoezi hilo kwenye mikoa waliyopangiwa kama ifuatavyo:

Kwa Mkoa wa Dar es salaam kutafanyika usafi wa fukwe utakaoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdori Mpango, Kwa Kanda ya Ziwa Mkoa wa Geita atakuwepo Waziri Mkuu wa Nchi Mhe.Kasim Majaliwa Majaliwa katika Hospital ya Chato, kwa Kanda ya Kati atakuwepo Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt.Dotto Mashaka Biteko, Nyanda za juu Kusini atakuwepo Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Tulia Akson, Kanda ya Kaskazini itaongozwa na Jaji Mkuu Tanzania Profes Ibrahim Juma na wakuu wa Mikoa kwenye mikoa yote nchi nzima.

Ameainisha pia katika wiki hiyo ya Mazingira kutazinduliwa sera ya Taifa ya uchumi wa buluu ya mwaka 2024 itakayoambatana na ugawaji wa vyeti kwa wadau wa mazingira na hundi kwa Halmashauri zitakazofanya vizuri