TAKA NGUMU NI FURSA KATIKA KUJIONGEZEA KIPATO –DKT GWAMAKA


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Dkt. Samuel Gwamaka ameikumbusha jamii juu ya kutenganisha taka ambazo zina oza na zisizo oza na pia kutokana na aina za taka. Ameeleza kuwa taka ni kitu ambacho hakiepukiki katika jamii yetu kwani kila siku katika maisha ya binadamu tunazalisha taka lakini ni muhimu tuweke utaratibu wa kuzisimamia ambao hautaharibu mazingira.

Dkt. Gwamaka ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo hii.Ameelezakuwa taka hizo zinazozalishwa ingawa zinaonekana ni vitu ambavyo havifai kwa matumizi tena,lakini ni malighafi ambazo zina weza kutumikakwa maendeleo ya viwanda hapa nchini.

“Taka ni fursa.Mfano wa taka ni, mabaki ya chakula, plastiki navyuma.Viwanda vinaweza kupata vyanzo vya malighafi kutoka kwenye taka,mfano taka za chuma zitapelekwa kwenye viwanda vya chuma, taka zenye mabaki ya chakula zitapelekwa kwenye madampo na huko wanaweza wakatengeneza mbolea pamoja na gesi kwa matumizi ya nyumbani. Lakini sio hivyo tu, kwa taka zinazotokana na maboksi na karatasi kuna viwanda vyenye kuzihitaji pia, badala ya kuagiza malighafi kutoka nje ya nchi. Hii itasaidia kiuchumi na pia katika utunzaji wa mazingira kwani kutakuwa na uzalishaji mdogo wa taka nchini.”

Ameendelea kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo kutakuwa na viwanda ambavyo vinapata malighafi kwa unafuu na urahisi hapahapa nchini.Utenganishaji wa taka utaboresha na kuimarisha uchumi wetu wa kati na vilevile azma ya kukuza viwanda inakuwa imekamilika.

“Nina waasa wananchi wajue kuwa taka ni fursa lakini ni pale tu zinapotengwa kuanzia pale zinapozalishwa.Pamoja na hayo, tumeshazielekeza Halmashauri za nchi nzima zianze mchakato wa kutenganisha taka. Mfano Halmashauri ya Mbeya imeshaanza na tunafanyanao kazi kwa pamoja. Halmashauri zote za Miji tunawakaribisha NEMC njooni tutafanya kazi pamoja na nyinyi bega kwa bega kuhakikisha mnafanikiwa kuanzia kwenye tafiti kuhusu taka za aina gani zinazozalisha katika eneo husika mpaka jinsi ya kuzitenganisha, kwani Baraza lipo kwa ajili yenu. Tuna kanda nane nchi nzima naziko tayari kushirikiana na nyinyi kufikia azma hiyo”

Aidha Dr. Gwamaka ameeleza kuwa Sheria ya Mazigira ya 2004 imezipa Halmashauri za Miji jukumu la kusimamia taka ikiwa pamoja na kufaya tafiti kwenye maeneo yao kufahamu aina gani ya taka zinazozalishwa.

Kama inavyofahamika kwenyeMijikuna taka tofauti zinazalishwa kutoka mahospitalini, sokoni, viwandani, shuleni na majumbani n.k. hivyo Halmashauri zinapaswa kujua aina ya taka na kiasi kinachozalishwa katika eneo lake kuanzia kwenye vyanzo.

“Kama Halmashauri zitatambua aina na kiasi cha taka kinachozalishwa katika eneo lake ni rahisi kutenganisha taka hizo kwa kuyapa rangi tofauti tofauti mapipa au vizimba vinavyokusanya aina tofauti ya taka hizo, hii itasaidia kutambua taka hatarishi na zisizo hatarishi na ambazo zinaweza kurejelezwa” amesema Dkt. Gwamaka.

Aidha Dkt. Gwamaka ameendelea kusisitiza kuwa kuna haja ya kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili wajue kuwa hizi taka zinaweza kuwapa watu ajira na kuongeza kipato. Pamoja na hayo kama wananchi wakitenganisha taka itasaidia pia kutunza mazingira na kuwa na wananchi wenye afya bora.