​𝐖𝐀𝐙𝐈𝐑𝐈 𝐃𝐊𝐓. 𝐀𝐒𝐇𝐀𝐓𝐔 𝐊𝐈𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐀𝐙𝐔𝐑𝐔 𝐁𝐀𝐍𝐃𝐀 𝐋𝐀 𝐍𝐄𝐌𝐂 𝐌𝐀𝐎𝐍𝐄𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐍𝐀𝐍𝐄𝐍𝐀𝐍𝐄-𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) azuru Banda la NEMC Maonesho ya Kimtaifa ya Kilimo (Nanenane) katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma na kupatiwa elimu ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Dkt. Kijaji alipozungumza kwenye banda hilo katika Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo " chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi" amesema suala la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira ndio msingi pekee wa kuhakikisha hayo yanatekelezeka.

"NEMC jukumu lenu kubwa ni kuishauri Serikali namna bora ya kuenenda katika kusimamia mazingira, hivyo ninyi mjikite sana kwenye kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi, hasa ikizingatiwa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ndio uti wa mgongo wa Serikali, mkifanya hivyo hayo mengine yote yataenda kwa utaratibu unaopaswa na matokeo chanya yataonekana" amesema Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).