TAIFA LIMEPATA MUAFAKA TATIZO LA UTUPAJI CHUPA ZA PLASTIKI –Mh. ZUNGU


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na MazingiraMhe. Mussa Azzan Zungu amefaya ziara katika kiwanda cha Sunda Fiber Limited kilichopo kata ya kilangalangawilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani, ili kujionea uzalishaji wa kiwanda hicho kama kinafanya uzalishaji wake kwa kuzingatia sheria na kanuni za Mazingira.

kiwanda hiki kinajishughulisha na uzalishaji wa kamba za kufungia mizigo na kutengeneza mito ya kulalia kwa kutumia malighafi ya chupa za plastic zilizotumika. Hiki ni kiwada kikubwa na pekee kilichopo Afrika Mashariki na Kati ambacho kinazarisha bidhaa zake kwa kutumia chupa zilizotumika kuwa bidhaa tena.

Katika ziara hiyo Mhe. Zungu aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Martin Ntemo, Meneja wa NEMC kanda ya Mashariki Bw. Arnold Mapinduzi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa pamoja na kikosi kazi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, NEMC pamoja na wadau wa Mazingira kutoka ng’os ya ECCT na Save the Coast.

Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Zungu ameeleza kuwa kiwanda hiki kinasaidia sana kusafisha Mazingira yetu kwa kurejeleza chupa za plastiki zilizotumika kugeuzwa kuwa bidhaa na kutumika tena, lakini hata hivyo ameeleza kuwa ifanyike juhudi ya ziada kwa kiwanda hiki pamoja na wadau wake Coca cola na peps kuweka maeneo maalum Nchi nzima ambayo chupa hizo zitakusaywa kabla ya kupeleka kiwandani.

“hii ni fursa kwa watanzania kujipatia kipato na kutunza Mazingira yetu kwa kutotupa chupa hovyo ambazo zimekwisha tumika, hivyo nimewaagiza Coca cola na wote wanaozalisha chupa za plastiki wawe na vituo vya kukusanyia chupa hizo kweye majiji yote Tanzania.” alisema Mhe. Zungu

Kwa upande wake muwakilishi wa Coca Cola Bw. Hajji Mzee amesema kuwa kiwanda hiki ni kiwanda pekee Afrika Mashariki na kati kinachoweza kuchakata chupa za plastiki zilizotumika kugeuza kuwa bidhaa na malighafi ambazo pia husafirishwa kwenda Nchi jirani. Alieleza hayo akiwa kiwadani hapo.

“Taifa letu limepata muafaka wa tatizo la utupaji wa chupa za plastiki zilizotumika, hivyo tutoe ushirikiano katika kiwanda hiki ili kufikia malengo yetu ya utunzaji wa Mazingira katika Nchi yetu”.

Aidha Mh. Zungu ameeleza kuwa japo kiwanda hiki kinatunza Mazingira kwa kukusanya chupa zilizotumika ambazo zina athari kubwa kimazingira lakini wahakikishe wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na sera za Nchi.

Hata hivyo katika ziara yake Mh. Zungu ametembelea kiwanda cha Gravita Tanzania Ltd kilichopo Zegereni Kibaha mkoa wa Pwani kujionea namna wanavyofanya shughuli zao bila kuathiri Mazingira na kuvunja Sheria ya Nchi. Kiwanda hiki kinajishughulisha na utengenezaji wa malighafi ya shaba ambayo inatumika kuzalisha bidhaa ya masufuria, waya na bidhaa zote zinazotengenezwa kwa kutumia shaba. Hata hivyo Mh. Zungu alipata nafasi ya kapanda mti katika kiwanda hiko wakati wa ziara hiyo.

Kwa upande wake Bw. Arnold Mapinduzi Meneja wa Kanda ya Mashariki (NEMC) ameeleza kuwa kiwanda cha Gravita kina cheti cha Mazigira lakini kibali cha ukusayaji wa taka hatarishi ya vyuma chakavu kimeisha muda wake “Natoa rai kwa wenye viwanda, kibali cha ukusanyaji, usafirishaji na uhifadhi wa vyuma chakavu kinapokaribia kuisha muda wake unatakiwa kuomba mapema kuepuka usumbufu.” alisema Bw. Mapinduzi

Aidha Mhe. Zungu ametembelea kiwanda cha Kiluwa Steel Group Compay ltd kilichopo kata ya Kilagalanga, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani alikagua kiwanda hiko kujionea namna wanavyofanya shughuli zao bila kuvunja Sheria, katika ziara yake amebaini kuwa kiwanda hiki kina kibali cha Mazingira lakini kibali cha ukusanyaji wa taka hatarishi ya vyuma chakavu hawana.

“ninawaagiza NEMC kwa kushurikiana na watumishi wa Mkoa na Wilaya kuja kukagua kiwanda hiki ili kupata taarifa zilizo sahihi.” Mhe. Zungu alimalizia kwa kusema.