Karibu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Baraza lilianzishwa kwa Sheria ya Taifa ya Usimamizi wa Mazingira Na. 19 ya mwaka 1983 kama chombo cha kuishauri serikali juu ya masuala ya utunzaji endelevu wa mazingira. Baraza lilianza kazi rasmi mwaka 1986 na baadaye kupewa nguvu ya kisheria ya kusimamia hifadhi ya mazingira nchini kwa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004.
Majukumu ya Baraza ni kutekeleza shughuli za uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; kusimamia mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) pamoja na ukaguzi wa mazingira; kufanya tafiti za mazingira; kujenga uelewa wa mazingira kwa umma na kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Sheria nyingine zozote zilizoandikwa.