KANDA YA KASKAZINI

UTANGULIZI

Kanda ya Kaskazini ni moja kati ya Kanda 13 za Baraza la Taifa la HIfadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2005 ambapo kuanzishwa kwake ni lengo la Baraza kusogeza huduma karibu zaidi na jamii na kuihudumia jamii kwa ufanisi na uwazi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu huku ikilenga kusimamia Uhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

Kanda hii inahudumia Mikoa mitatu ambayo ni Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambapo Makao makuu ya Kanda hiyo yanapatikana katika Mkoa wa Arusha, Makutano ya Barabara za Makongoro – Goliondoi Jengo la Kituo cha Utalii cha Ngorongoro.

Kanda ya Kaskazini imebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii na Mifumi Ikolojia nyeti yenye umuhimu Kitaifa na Kimataifa. Maeneo haya ni pamoja na Maeneo yaliyohifadhiwa kama vile Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Hifadhi za Taifa za Tarangire, Mkomazi, Kilimanjaro, Ziwa Manyara na Arusha. Hii pia inahusisha maeneo kadhaa yanayohifadhiwa kama vile Mapori Tengefu, Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii na Misitu ya Hifadhi.

Aidha pia unapatikana Mlima mrefu kuliko yote Barani Afrika (Kilimanjaro) wenye urefu wa Mita 5985 kutoka usawa wa Bahari. Pia kuna uchimbaji wa vito mbalimbali vya thamani ambapo miongoni mwao ni madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Tanzania pekee.

MAJUKUMU YA KANDA YA KASKAZINI

  • Kuratibu na kuunganisha vyombo mbalimbali vya Serikali katika masuala yanayohusiana na Usimamizi na Uhifadhi wa mazingira kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 na Kanuni zake

  • Kuongeza uelewa kwa umma kuhusu masuala ya Usimamizi wa Mazingira

  • Kuhakikisha kunakuwa na Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.

  • Kuhakikisha miradi ya maendeleo kabla ya kutekelezwa inafanyika Tathmini ya Athari kwa Mazingira au kwa iliyopo inafanyiwa Ukaguzi wa Awali wa Mazingira, ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio ya miradi hiyo ili kupata Cheti cha Mazingira;

  • Kushughulikia Malalamiko, Matukio na Maoni mbalimbali yanayohusu Mazingira yanayowasilishwa Ofisini

  • Kutoa miongozo kwa jamii kuhusiana na masuala mbalimbali ya Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira

  • Kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayohusu Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira na Maliasili.

  • Kutoa elimu ya Utunzaji wa Mazingira kwa umma kupitia vyombo vya Habari mfano; Radio, televisheni na magazeti.

  • Kuendesha na kuratibu tafiti mbalimbali zinazohusu Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira

MIRADI INAYOSIMAMIWA NA KANDA YA KASKAZINI

NEMC Kanda ya Kaskazini inasimamia Sera na Sheria za Mazingira, Ofisi hii inahakikisha kuwa uchumi wa Nchi unakua sambamba na Uhifadhi wa Mazingira. Hivyo, kusimamia Utunzaji wa Mazingira katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo;

Miradi ya huduma za afya ; Kanda ya kaskazini inasimamia jumla ya miradi ya afya 1286

Miradi ya shughuli za kiutalii ni 317

Miradi ya nishati ni 247

Miradi ya viwanda vya mbao ni 201

Miradi ya uwekezaji katika viwanda 176

Miradi ya kilimo ni 118

Miradi ya ghala za kuhifadhia bidhaa, vifaa au mali nyingine ni 74

Miradi ya ujenzi ni 27

Miradi ya uchimbaji wa madini ni 26

Miradi ya wakulima wa mifugo ni 12

Miradi ya ujenzi wa majengo ni 11

Miradi ya mawasiliano ni 5

Miradi ya miundombinu ni 3



MAFANIKIO MAKUBWA YA KANDA YA KASKAZINI

NEMC Kanda ya Kaskazini imefanikiwa kusimamia Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa miradi mikubwa kama barabara, viwanda na migodi

NEMC Kanda ya Kaskazini imefanikiwa kuendesha program mbalimbali katika vyombo vya Habari kwa lengo la kutoa elimu kwa Umma, fursa zilizopo katika Mazingira na Utunzaji wa Mazingira na majukumu ya Baraza la kwa ujumla

NEMC Kanda ya Kaskazini inaandaa shughuli mbalimbali za kufanya usafi wa Mazingira na upandaji wa miti.