KANDA YA TEMEKE

UTANGULIZI

Kanda ya Temeke ni moja ya kanda 13 za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) inayosimamia Wikaya ya Temeke iliyopo mkoa wa Dar es Salaam. Kanda hii ya Temeke ilianzishwa mwezi Julai, 2022 ikiwa na jukumu la kutoa huduma ya udhibiti na usimamizi wa mazingira katika Wilaya ya Temeke. Kanda ya Temeke ina ukubwa wa kilometa za mraba takribani  656.

OFISI ZILIPO

Ofisi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Temeke kwasasa tupo eneo la Mikocheni, Mtaa wa Regent, Jijini Dar es Salaam. Tunatarajia hivi karibuni kuhamia jengo la PSSSF(Quality Plaza) lililopo eneo la Banda la Ngozi, Barabara ya Nyerere, Mkoa wa Dar eS salaam kwa ajili ya kutoa huduma ya karibu kwa wateje wetu.

NGUVU YA KANDA

Eneo linalosimamiwa na Ofisi ya kanda ya Temeke lina Kata 23 na Mitaa 142 na lina jumla ya wakazi 1,346,674 kwa mujibu wa sensa ya Mwaka 2022. Kiujumla Kanda ya Temeke imekuwa ni kivutio cha watu wengi kwa kufanya shughuli kubwa tatu za za kiuchumi kama viwanda, maghala ya kutunzia mizigo kwa ajili ya kuhudumia viwanda, bandari ya Dar es Salaam na masoko ya Tandika na Kariakoo na  uwepo wa ongezeko la Bandari kavu ndogo (ICDs) zinazopokea mizigo kutoka bandarini ya Dar es Salaam. Shughuli nyingine ni pamoja na uwepo wa biashara kubwa na ndogo katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Temeke yakiongozwa na soko la Tandika. Pia kuna ujenzi wa nyumba za biashara na makazi cha wastani, hali ambayo inaendelea kufanya mabadiliko ya kiuchumi, kimazingira na kijamii. 

Aidha, vivutio vya kipekee kwa Kanda ya Temeke ni pamoja na uwepo wa sehemu kubwa ya Bandari ya Dar es Salaam ndani ya Kanda yetu ambayo inahudumia watanzania ikiwa ni pamoja na wageni kutoka nchi jirani. Kivutio kingine ni uwepo wa uwanja mkubwa wa Mpira wa Benjamini Mkapa ni kivutio cha pekee ambacho kinawavutia wenyeji na wageni kutoka mikoa na wilaya majirani kuja kutazama mpira wa miguu. Pia Daraja na Mwalimu Nyerere linalounganisha Wilaya ya Temeke na Kigamboni limekuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni wanaokuja Dar es Salaam.

MAJUKUMU YA KANDA 

  • Ofisi ya Kanda inamwakilisha Mkurugenzi Mkuu katika kutekeleza Sheria ya Mazingira Sura 191. Majukumu mahsusi ni pamoja na:
  • Kukuza uelewa kuhusu sheria ya mazingira kwa wadau
  • Kuhakikisha uzingatiaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira
  • Kuratibu mchakato wa tathmini ya athari kwa mazingira (TAM)
  • Ufuatiliaji wa mazingira na mifumo ikolojia
  • Kuhakikisha changamoto za mazingira zinapatiwa ufumbuzi wa njia ya tafiti na uanzishwaji wa miradi ya kimazingira
  • Uratibu wa shughuli za mazingira kwa shughuli za kisekta na wadau mbalimbali
  • Kuhakikisha shughuli zinginezo zinazotakiwa kufanywa na Baraza chini ya Sheria ya Mazingira ya Sura Na. 191 zinatekelezeka       

MAWASILIANO

Unaweza kufika au kuwasaliana na Ofisi kwa anuani ifuatayo:

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) – Kanda ya Temeke, Jengo la PSSSF (Quality Plaza), S.L.P. Dar es Salaam, TANZANIA.

Simu (Meneja): +255784506267

Barua pepe (Meneja): abel.sembeka@nemc.or.tz