KANDA YA MOROGORO RUFIJI
UTANGULIZI
Kanda ya Morogoro-Rufiji ipo katika Manisapaa ya Morogoro, Jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ghorofa ya pili, mkabala na kituo cha mabasi cha zamani. Ina eneo la kilomita za mraba 80,049 ikihudumia na kusimamia Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro pamoja na Wilaya ya Rufiji katika Mkoa wa Pwani.
MAJUKUMU YA KANDA
- Kuratibu Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa miradi ya maendeleo.
- Kufanya Kaguzi za mazingira.
- Kufanya na/au kuratibu Tafiti za Mazingira;
- Kufuatilia na kuhimiza Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; na
- Kutoa elimu ya mazingira kwa umma.
NGUVU YA KANDA
Ni Kanda yenye utajiri wa Milima na Mabonde yanayowezesha ardhi nduzi ya Kilimo cha mazao anuwai ikiwa ni pamoja na Mahindi, Miwa, Maharage, Mpunga, Minazi, Korosho, Matunda na Viungo. Ni Kanda yenye maji mengi yanayotokana na mito, vijito na Chem chemu ambapo mito mikubwa ya Kilombero, Rufiji na Wami inapita ndani yake. Wakati Bonde la Rufiji (Kilombero na Rufiji yenyewe) ni muhimu kwa ajili ya kufua umeme, Bonde la Wami/Ruvu ndilo linalowezesha upatikanaji wa maji kwa ajili ya Mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam.
Uwepo wa mito hii unaipa kanda upekee katika kuchangia umeme wa taifa kwani mabwawa muhimu ya umeme ya Mwalimu Nyerere, Kidatu na Kihansi yapo katika kanda hii.
Vivutio: Kanda ya Morogoro-Rufiji imejaaliwa utajiri wa vivutio vya utalii kama vile Mbuga za Wanyama za Mikumi, Nyerere na Udzungwa; Hifadhi ya Wanyama ya Selous; Milima ya Uluguru; pamoja na Maporomoko ya Maji kama yale ya Kinole, Sanje na Choma.
Kanda hii inayo madini mengi ikiwa ni pamoja na dahabu, vito na madini ujenzi vikiwemo kokoto na mchanga. Ni Kanda iliyojaaliwa kuwa na miundombinu muhimu ya usafiri ikiwa ni pamoja na barabara (Dar - Dodoma, Dar - Mbeya) na reli (MG na SGR) yote hii inapita katika Kanda hii.
Viwanda vikubwa katika Kanda hii ni pamoja na vile vya Sukari vya Mtibwa, Kilombero na Mkulazi; kiwanda cha nguo cha “21st Century”, Kiwanda cha Ngozi na Kiwanda cha kukoboa Mpunga cha Wilma
Mawasiliano:
NEMC – Kanda ya Morogoro Rufiji,
Jengo la NHC 2D Complex ghorofa ya 2,
Barabara ya zamani ya DSM,
S. L. P,
Morogoro, TANZANIA.
Simu: +255 738787;
Barua pepe: nemcmorogoro@nemc.or.tz.