KANDA YA BAGAMOYO
UTANGULIZI
Kanda ya Bagamoyo (BZ) ilianzishwa mwezi Julai, 2023 ikiwa na eneo la jumla la kilomita za mraba 28,293 kwa lengo la kuhudumia Wilaya 11 ambazo ni Bagamoyo na Chalinze katika mkoa wa Pwani, na Jiji la Tanga, Lushoto, Bumbuli, Mkinga, Pangani, Muheza, Korogwe, Kilindi, na Handeni katika mkoa wa Tanga. Lengo kuu la kuanzishwa kwa Kanda hii ni kusogeza huduma za Baraza karibu na jamii inayodhibitiwa. Kanda hii inajumuisha mifumo mbalimbali ya ikolojia ikiwemo ya majini (maji baridi na bahari), na ya nchi kavu kuanzia maeneo ya milima hadi maeneo ya tambarare. Shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo, uvuvi, usafirishaji,viwanda,utalii na uchimbaji wa madini.
MAJUKUMU YA KANDA
Majukumu ya kanda hii yamelenga hasa utekelezaji wa masuala yanayohusiana na usimamizi na uhifadhi wa mazingira kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Mazingira EMA CAP 191 na Kanuni zake. Majukumu haya ni pamoja na kuhakikisha
· Uzingatiaji wa sheria za mazingira na utekelezaji wake katika maeneo mbalimbali na miradi ya maendeleo,
· Uzingatiaji wa tathmini ya athari kwa mazingira na ukaguzi,
· Kushughulikia maswali na malalamiko ya mazingira,
· Kutoa mwongozo kwa wateja kuhusu masuala ya usimamizi na uhifadhi wa mazingira,
· Kutoa elimu na kuongeza uelewa, na kusimamia utekelezaji wa shughuli zinazohusiana na usimamizi na uhifadhi wa rasilimali na mazingira.
NGUVU YA KANDA
Kanda ya Bagamoyo imezungukwa na vivutio mbalimbali vya utalii ambavyo ni: Hifadhi za Taifa za Saadani na Mkomazi, Milima ya Usambara, Mapango ya Amboni, Hifadhi ya Viumbe Hai ya Irente, Maporomoko ya maji ya Soni, Magofu ya Kaole, Jengo la Kijerumani (German Boma), Mji wa Kale wa Bagamoyo, Makumbusho ya Caravan Serai, Makumbusho ya Bagamoyo, Makumbusho ya Misheni ya Kikatoliki na Makumbusho ya Urithi Tanga.
MAWASILIANO
Bi. Ndimbum Joram ni Meneja wa kanda ya Bagamoyo na anapatikana kwa mawasiliano yafuatayo;
35 Regent Street,
P.O. Box 63154, 11404 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2774852; +255 754 088 325; +255 22 2774889; +255 713 608 930 / 735 608 930
Fax: +255 22 2774901
Email: nemcbagamoyo@nemc.or.tz
Website: www.nemc.or.tz
Simu: 0753 402334.