KANDA YA ILALA

UTANGULIZI

Kanda ya Ilala ni miongoni mwa Ofisi za Kanda za NEMC zilizopo katika Jiji la Kibiashara la Dar es Salaam. Ofisi ya Kanda iko ndani ya Ofisi za NEMC zilizoko Mikocheni, 35 Regent Estate. Kanda hii inahusisha Mamlaka ya Jiji la Dar es Salaam, ambayo hapo awali ilijulikana kama Manispaa ya Ilala. Kanda hii Inaundwa na kata 36 na Tarafa saba, ambazo ziko chini ya uongozi wa Maafisa Mazingira (DEMOs) kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

 

NGUVU KUU YA KANDA

Kanda ya Ilala imezungukwa na fursa mbalimbali zinazotokana na Jiji la Dar es Salaam kuwa lango kuu la biashara. Fursa hizo ni pamoja na:

·       Reli ya Standard Gauge (SGR)

·       Mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka  (BRT)

·       Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi (LMBDP)

·       Soko la Kariakoo

·       Mamlaka ya Bandari

·       Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA)

·       Uwekezaji katika majengo mbalimbali makubwa na madogo, viwanda vya aina tofauti, shule, kumbi za starehe, hoteli, vituo vya mafuta na nyinginezo.

 MUHTASARI WA KANDA

Kanda ya Ilala ilianza rasmi shughuli zake mwezi Julai 2023 ikiwa na lengo la kuleta huduma karibu zaidi na wananchi na kushughulikia masuala yote yanayohusiana na mazingira kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu ndani ya mamlaka ya Jiji la Dar es Salaam. Kanda hii inaongozwa na Meneja wa Kanda na inajumuisha maofisa pamoja na watumishi wasaidizi.

 

MAJUKUMU YA KANDA:

·       Kuratibu na kuunganisha taasisi mbalimbali za serikali kuhusu masuala yanayohusiana na usimamizi wa mazingira, ikiwemo kufuatilia uzingatiaji wa Sera, sheria, kanuni na Miongozo ya  mazingira na utekelezaji wa miradi na mipango mbalimbali;

·       KupitiaTathmini ya Athari ya Mazingira (EIA) na kufanya ukaguzi wa mazingira kwa miradi iliyowasilishwa ndani ya kanda;

·       Kukusanya ada na tozo za mazingira za kila mwaka;

·       Kuhamasisha wadau kuhusu usimamizi bora wa mazingira;

·       Kujibu malalamiko yote yanayowasilishwa ndani ya kanda;na

·       Kutoa msaada wa kiufundi na mwongozo kuhusu usimamizi wa mazingira na rasilimali asilia, pamoja na kutekeleza majukumu mengine kama yanavyoainishwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Sura ya 191).

  MAWASILIANO

35 Regent Street,
S.L.P  63154, 11404 Dar es Salaam
SIMU: +255 22 2774852; +255 754 088 325; +255 22 2774889; +255 713 608 930 / 735 608 930
Fax: +255 22 2774901
Barua pepe: nemcilala@nemc.or.tz
Tovuti: www.nemc.or.tz