KANDA YA MASHARIKI KASKAZINI
1.0 UTANGULIZI
Kanda ya Mashariki Kaskazini ni miongoni mwa kanda kumi na tatu (13) za Baraza zilizopo nchini. Kanda hii inashughulika na Manispaa mbili (Kinondoni na Ubungo) za Mkoa wa Dar es Salaam; na Wilaya ya Kibaha iliyoko Mkoa wa Pwani. Kanda ina ukubwa wa kilometa za mraba 2,582.58. Kanda inapakana na Wilaya ya Bagamoyo kwa upande wa Kaskazini; upande wa Magharibi imepakana na Wilaya ya Chalinze; Mashariki imepakana na Bahari ya Hindi na upande wa Kusini imepakana na Jiji la Dar es Salaam (zamani ikijulikana kama Manispaa ya Ilala).
2.0 ENEO LA KANDA
Kanda ina ukubwa wa kilometa za mraba 2,582.58. Kanda inapakana na Wilaya ya Bagamoyo kwa upande wa Kaskazini; upande wa Magharibi imepakana na Wilaya ya Chalinze; Mashariki imepakana na Bahari ya Hindi na upande wa Kusini imepakana na Jiji la Dar es Salaam (zamani ikijulikana kama Manispaa ya Ilala).
3.0 MAJUKUMU YA KANDA
NEMC Kanda ya Mashariki Kaskazini ilianzishwa kwa madhumuni ya kutelekeza majukumu na huduma za Baraza karibu na jamii za wilaya iliyo ndani ya kanda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu. Hivyo, Kanda hutekeleza majukumu yafuatayo: -
(i) Kusimamia mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) au Ukaguzi wa Mazingira (Kuratibu, kufanya mapitio ya ripoti za TAM au Ukaguzi wa Mazingira kutoka kwa wenye miradi na kufuatilia utekelezaji wake) kwa mujibu wa sheria ili kupata vyeti stahiki.
(ii) Kutekeleza shughuli za uzingatiaji na utekelezaji (compliance and enforcement) wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
(iii) Kutoa ushauri wa kitaalam kwa mamlaka mbalimbali za serikali zilizopo katika kanda kuhusu hifadhi na usimamizi wa mazingira na kusaidia taasisi na asasi mbali mbali zinazoshughulika na usimamizi wa maliasili na mazingira.
(iv) Kuendesha programu za utoaji wa Elimu ya Mazingira kwa umma kupitia vyombo vya Habari na matukio mbalimbali ya Kitaifa.
(v) Kushughulikia Malalamiko, Matukio na Maoni mbalimbali ya Jamii yanayohusu Mazingira.
(vi) Kuendesha na kuratibu tafiti mbalimbali za usimamizi wa mazingira
(vii) Kufanya shughuli nyingine zozote kwa maagizo ya Mkurugenzi Mkuu wa Baraza au Waziri Mwenye dhamana ya Mazingira nchini
4.0 MAWASILIANO (MAHALI OFISI ZA KANDA ZILIPO)
KANDA YA MASHARIKI KASKAZINI
MENEJA: GLORY J. KOMBE
MAWASILIANO:
Simu ya Kiganjani: 0782 370155
Barua pepe: glory.kombe@nemc.or.tz