Wasifu
Dr. Immaculate Sware Semesi, anahudumu kama Mkurugenzi Mkuu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu. Dr. Immaculate Sware Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu. Mbali na wadhifa huo Dr. Immaculate Sware Semesi, amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 5 mwaka 2015/2020. Pia amewahi kuwa Mjumbe wa wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Dr. Immaculate Sware Semesi, amewahi kuwa Mjumbe wa kamati ya kuchunguza masuala ya kiuchumi na kisheria kuhusu usafirishaji wa Makinikia iliyoongozwa na mwenyekiti wake Profesa Nehemiah Osoro. Kamati hiyo iliibua uozo uliokuwepo kwenye Mikataba ya Madini, huku ikifichua kutosajiliwa kwa kampuni ya Acacia Mining iliyojinasibisha kuwa ni mmiliki wa kampuni za Bulyanhulu Gold Mines, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals.
Uzoefu wake Kitaaluma Dr. Immaculate Sware Semesi, pamoja na hayo amewahi kuwa Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kipindi cha takribani miaka 10 katika masuala ya Utafiti wa Bahari. Pia aliwahi kufanya kazi katika Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kama Afisa Mazingira Mkuu I.
Dr. Immaculate Sware Semesi, alipata Shahada ya kwanza ya Sayansi katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Tanzania. Alipata Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kilimo nchini Norway. Pia alijipatia Shahada ya Udaktari (PHD) ya Filosofia katika Chuo Kikuu cha Stockholms mwaka 2009 nchini Sweden.