USAJILI NA UTENDAJI WA WATAALAM ELEKEZI WA MAZINGIRA
1 MFUMO WA USAJILI NA MAOMBI YA CHETI CHA UTENDAJI KWA WATAALAMU ELEKEZI MTANDAONI
Mfumo huu unawezesha Washauri Elekezi wa Mazingira kuona na kufanyia kazi miradi waliyohusishwa kupitia akaunti zao badala ya akaunti za wawekezaji au wenye miradi. Hata hivyo, Mshauri Elekezi hataweza kufuta au kuhuisha taarifa bali ataweza kutekeleza yafuatayo:
i. Kuangalia miradi aliyokabidhiwa
ii. Kuweka nyaraka mbalimbali baada ya kuidhinishwa na mwenye mradi
1.1 Malengo ya mfumo wa mtandaoni wa usajili wa Washauri Elekezi
i. Kuongeza ufanisi
ii. Kupata taarifa sahihi za Washauri Elekezi
iii. Utunzaji bora wa taarifa
iv. Kutenganisha majukumu ya mwekezaji na Mshauri Elekezi
v. Ufanisi katika kukusanya mapato
1.2 Hatua za usajili kwa Washauri Elekezi wa Mazingira binafsi na kampuni
Hatua ya kwanza: Fungua akaunti kupitia tovuti ya Baraza la Hifadhin a Usimamizi wa Mazingira kipengele cha ‘EIA online system’ au moja kwa moja kupitia https://eia.nemc.or.tz/
Bofya kipengele kinachosoma ‘Expert’
- Endapo una akaunti, ingiza jina la akaunti yako na nywila ‘signin’
- Endapo ni mtumiaji wa mara ya kwanza, jisajili ‘signup’. Kampuni za Washauri Elekezi zinapaswa kufungua akaunti ya kampuni sio za watu binafsi.
- Baada ya kusajili, utapokea ujumbe kupitia barua pepe uliyotumia katika usajili ambapo unatakiwa kubofya kiungo ‘link’ kwenye ujumbe huo ili kuamsha akaunti yako.
Hatua ya pili: Baada ya kuamsha akaunti yako mfumo utakuruhusu kuingia na kufanya maombi ya usajili
Hatua ya tatu: Jaza taarifa zako binafsi
Hatua ya nne: Chagua kipengele kinachosoma ‘Registration of individual au Firm of Experts’
Hatua ya tano: Endelea na usajili kwa kujaza maeneo yote ya fomu ya maombi ya usajili na kuweka nyaraka husika kwa mujibu wa Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Usajili na Utendaji wa Washauri Elekezi za Mwaka 2021
Kumbuka: Kampuni za Washauri Elekezi zinapaswa kutengeneza ushirikiano (partnership) wa Wataalamu Elekezi angalau wawili wenye cheti cha Utendaji ambao wataanishwa na kujulikana kama ‘Lead Experts’. Wataalumu hao watapokea ujumbe unaotaka kukubali au kukataa umoja huo.
Hatua ya sita: Baada ya kukamilisha taarifa zote na kulipa ada, maombi yanaweza kuwasilishwa
i. Kusudio la mfumo wa usajili kupitia mtandao
- Kupunguza malalamiko kutoka kwa wawekezaji dhidi ya Washauri Elekezi
- Kuwapunguzia kazi wafanyakazi wa Baraza
- Kuongeza uwajibikaji
- Kupata taarifa sahihi za Washauri Elekezi
1.3 Hatua za maombi ya cheti cha utendaji kwa Washauri Elekezi binafsi na Kampuni
Hatua ya kwanza: Ingia katika akaunti yako
Hatua ya pili: Chagua ‘Categorization of individual au Firm of Experts’
Hatua ya tatu: Jaza maelezo katika fomu na kuweka nyaraka husika kwa mujibu wa Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Usajili na Utendaji wa Washauri Elekezi za Mwaka 2021
Angalizo: Kampuni za Washauri Elekezi wenye vyeti visivyo vya mfumo, yaani, ‘manual’ wanapaswa kuhuisha taarifa zao za kampuni kwa kuingia kwenye ‘registration’ na kuomba ushirikiano (partnership) kabla ya kuendelea na maombi ya cheti cha utendaji. Uhuishaji huo utaruhusu kampuni kuanisha Washauri Elekezi angalua wawili watakojulikana kama ‘Lead Experts’ kwa utaratibu uliyoainishwa hapo chini:
- Fungua kipengele cha ‘Registrations’ kwa kubofya ‘View’
- Katika taarifa za usajili, tafuta kipengele kilochoandikwa ‘Firm’ halafu bofya.
- Tafuta kipengele cha ‘Add Expert’ halafu bofya.
- Dirisha ‘window’ lingine linatofunguka kwa ajili ya kuingiza taarifa za Washauri Elekezi ‘Lead Experts’ na ‘normal’
- Jaza taarifa husika za kila Mshauri Elekezi halafu hifadhi ‘save’ au ‘Add’ kukamilisha mchakato.
Angalizo: Hakikisha unachagua angalau ‘Lead Expert’ wawili kwa ajili ya kampuni
Hatua ya nne: Baada ya kukamilisha taarifa zote na kulipia, maombi yako yanaweza kuwasilishwa
2. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
i. Kwa mujibu wa kifungu cha 82 na 230h cha Sheria (Sura 191) kikisomwa kwa pamoja na kanuni ya (14A ya GN.No.474/2018) pindi mradi utakapokuwa umesajiliwa na hakuna hatua zozote zitakazoendelea kwa upande wa mwekezaji kwa kipindi cha miaka miwili, mradi huo utaondolewa kwenye usajili na mhusika atatakiwa kusajili upya
ii. Maombi ya usajili na cheti cha Utendaji kwa Washauri Elekezi wa Mazingira utafanyika kwa kuzingatia Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Usajili na Utendaji wa Washauri Elekezi za Mwaka 2021 pamoja na marekebisho ya mwaka 2022
iii. Ikiwa unahitaji msaada wa kiufundi au maelezo zaidi Andika kwa eiasupport@nemc.or.tz
ORODHA YA WATAALAM ELEKEZI WA MAZINGIRA
Orodha ya Wataalamu binafsi na kampuni Elekezi za Mazingira zinazostahili kuandaa taarifa za Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Ukaguzi wa Mazingira (TAM/UM) inaweza kupatikana au kupakuliwa kupitia kiungo kifuatacho:
[https://mma.nemc.or.tz/pms/eligible-expert?q=]