Uendeshaji tafiti mazingira

Kurugenzi hii ina jukumu la kufanya tafiti, kuandaa maandiko na kutekeleza miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kulisaidia Baraza na Serikali kutoa maamuzi sahihi kwenye masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa kuzingatia matokeo ya utafiti, taarifa na takwimu zilizopo. Aidha, Kurugenzi imepewa dhamana ya kuratibu na kuelekeza utekelezaji wa Agenda ya Taifa ya Utafiti wa Mazingira (NERA), Usimamizi wa Mifumo ya Mazingira na masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi. Kurugenzi hii inaongozwa na Mkurugenzi. Utekelezaji wa majukumu unafanyika chini ya Idara mbili zinazoongozwa na mameneja: 1) Idara ya Uratibu wa Tafiti za Mazingira na  na 2) Idara ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Maeneo Maalumu.