Eneo la Utekelezaji wa Sheria
Majukumu na Wajibu katika Kitengo cha Utekelezaji wa Sheria (Enforcement)
i. Kufanya ukaguzi wa mazingira, uchunguzi, na ufuatiliaji pamoja na kukusanya ushahidi;
ii. Kukusanya sampuli na kuziwasilisha kwenye maabara iliyoidhinishwa kwa ajili ya uchunguzi;
iii. Kurekodi na kunakili taarifa yoyote kwa njia yoyote ile kwa ajili ya kutoa kielelezo mbele ya mahakama;
iv. Kutoa adhabu za kiutawala na kisheria kwa wale wanaokiuka taratibu;
v. Kutoa mchango wa kitaalamu wakati wa uandaaji wa nyaraka za kisheria;
vi. Kutoa ushahidi na kuwasilisha vielelezo mbele ya mahakama;
vii. Kutoa mafunzo kwa wakaguzi wa mazingira walioteuliwa na kuidhinishwa;
viii. Kushughulikia malalamiko ya mazingira kutoka kwa umma na matukio yanayoripotiwa
ix. Kuratibu na kuchakata maombi ya vibali vya usimamizi wa taka hatarishi.