Kitengo cha TEHAMA na Takwimu

Kitengo cha TEHAMA & Takwimu kinaongozwa na Meneja.

Malengo ya Kitengo:

Kutoa ushauri na utaalam juu ya maendeleo na utumiaji wa teknolojia katika utoaji huduma bora na uchambuzi wa takwimu.

Shughuli za Kitengo:

  • Kuendeleza na kuendesha Mfumo wa Habari ya Mazingira (CEIS) na kuwezesha upatikanaji wa taarifa na habari kwa Umma;
  • Kukusanya, kuchambua na kutoa takwimu za mazingira kwa matumizi anuwai;
  • Kutengeneza habari za kijiografia kwa kutumia GIS na Remote Sensing kwa matumizi mbali mbali;
  • Kuendeleza na kutekeleza mkakati wa teknolojia ya habari na mawasiliano;
  • Kuendeleza na kusimamia tovuti ya Baraza;
  • Kuendeleza na kudhibiti mifumo ya data na kuhakikisha usalama wake;
  • Kutengeneza, kutunza na kuhifadhi miundombinu ya mfumo wa TEHAMA na kuhakikisha ushirikiano wa kiteknolojia na Taasisi zingine za Serikali pamoja na wadau;
  • Kutekeleza sera ya Serikali ya TEHAMA;
  • Uangalizi wa data za Baraza; na
  • Kusimamia Maktaba na huduma za kituo cha habari ya Baraza.