NEMC YAUNGANA NA TAASISI NYINGINE KUADHIMISHA SIKU MAALUMU YA MAZINGIRA MAONESHO YA SABASABA 2025

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMCJulai 6, 2025limeungana na Taasisi mbalimbali kuadhimisha Siku ya maalumu ya Mazingira iliyotengwa kwa mara ya kwanza kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) 2025.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja huku tukio hilo likibebwa na Kauli mbiu isemayo "Matumizi ya Nishati safi na utunzaji wa Mazingira Kwa ustawi wa Tanzania bora".
Akizungumza katika hotuba yake Mhe. Cyprian Luhemeja ameitaka siku hiyo ya tarehe 6 /7 itengwe rasmi kuwa siku maalumu ya Mazingira kila mwaka katika maonesho hayo kuanzia maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa (sabasaba).
Sambamba na hilo amesisitiza watanzania wote kutunza Mazingira kwa kuwa Mazingira yaliumbwa kwanza Kisha mwanadamu akaumbwa baadae ili ayatunze, ayahifadhi na kuyalinda.
"Hii duniani ilianza kwa kutengenezewa Mazingira, mwanadamu ameumbwa wa mwisho baada ya Mazingira kutengenezewa na mwanadamu alipoumbwa alipewa kazi ya kuyatunza na kuyahifadhi Mazingira lakini mwanadamu anayaharibu kwa uchafuzi na ukataji wa miti.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza Dkt. Immaculate Sware Semesi amewapongeza washindi wa Mazingira Challenge iliyofanyika siku kadhaa zilizopita ambayo ililenga kumpata balozi kinara waUtunzaji wa Mazingira na anayehamasisha utunzaji wa Mazingira kwa kupiga picha ya Mazingira safi yanayomzunguka na kuwasilisha NEMC Kwa ajili ya mashindano hayo.
Maadhimisho hayo yalipambwa na mabalozi wa Mazingira pamoja na watumbuizaji nguli akiwemo Mrisho Mpoto pamoja na Mr. Tree na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Menejimenti ya NEMC, TANTRADE, STAMICO, Wanawake na Samia, Shirika la PUMA pamoja na wananchi waliotembelea maonesho ya sabasaba.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15