Kurugenzi ya Tathimini ya Mazingira (DESIA)

Kurugenzi inaongozwa na Mkurugenzi

Lengo

Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya tathmini ya athari za kimazingira na kijamii za miradi mipya na iliyopo.

MAJUKUMU

  • Kusimamia mchakato wa usajili, na udhibiti wa tathmini ya athari kwa mazingira
  • Kujenga uwezo wa Wizara za kisekta na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika tathmini ya athari za kimazingira na kijamii
  • Kupitia na kuandaa miongozo na taratibu za kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Kijamii (ESIA) na Ukaguzi na kusambaza kwa wadau.
  • Kusimamia na kuratibu uchunguzi na uhakiki wa muhtasari wa mradi, ripoti za upeo na kuidhinisha hadidu Rejea za kufanya tafiti za ESIA na Ukaguzi wa Mazingira (EA).
  • Kuratibu mapitio ya ripoti za ESIA/EA na mikutano ya Kamati ya Ushauri ya Kiufundi ili kujadili ripoti zilizowasilishwa.
  • Kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohusiana na mapitio ya ripoti za ESIA/EA
  • Kuwezesha mchakato wa utoaji wa Vibali vya Muda kwa miradi inayohusiana na Viwanda
  • Kuratibu Mamlaka za Wilaya, Wizara za Kisekta na ushiriki wa Umma katika mchakato wa mapitio ya ESIA.