Kanda ya Kusini
Eneo Ofisi zilipo na Anuani ya Posta
Ofisi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kusini ziko katika Manispaa ya Mtwara Mikindani. Ofisi kwenye Barabara ya TANU karibu na Jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania.Mawasiliano ya Posta, Simu na Barua pepe ni kama ifuatavyo:
Meneja wa Kanda,
NEMC- Kanda ya Kusini,
S. L. P 1259,
Mtwara, Tanzania,
Simu: +255-23-233-4683
Barua pepe: nemcmtwara@nemc.or.tz
Huduma zinazotolewa na ofisi
Ofisi ya NEMC Kanda ya Kusini ilianza rasmi shughuli zake mwaka 2014 kwa lengo la kutoa huduma karibu zaidi kwa wadau. Ofisi ya Kanda inajishughulisha na masuala ya kukuza uelewa wa hifadhi ya mazingira kwa wadau; kufanya utafiti na mipango ya mazingira; usimamizi wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake; kusajili miradi ya uwekezaji na kusimamia mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na ukaguzi wa Mazingira, kutoa ushauri kwa wadau wa mazingira kuhusiana na usimamamizi wa mazingira na mali ya asili pamoja na shughuli zingine kama inavyoagizwa kwenye Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Ofisi pia inapokea maombi ya ukusanyaji, hifadhi, usafirishaji na uteketezaji wa taka hatarishi kwa ajili ya hatua za utoaji wa vibali vinavyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya mazingira.
Eneo la Linalohudumiwa na Ofisi ya Kanda
Kanda ya Kusini inashughulikia Mikao mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Kanda ya Kusini inazo Mamlaka za Serikali za Mitaa zipatazo 24 ambazo zinakadiriwa kuwa na ukubwa wa 149,229 km2. Kulingana na Sensa ya mwaka 2012. Kanda ya Kusini inakadiriwa kuwa na idadi ya watu 3,512,397. Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kanda ya Kusini ni kama ifuatavyo:
- Mtwara - Masasi DC, Masasi TC, Mtwara Mikindani MC, Mtwara DC, Nanyamba TC, Nanyumbu DC, Newala DC, Newala TC, Tandahimba TC na Tandahimba DC.
- Lindi - Kilwa, Lindi MC, Lindi DC, Liwale DC, Nachingwea DC na Ruangwa DC.
- Ruvuma -Mbinga DC, Mbinga TC ,Namtumbo DC, Madaba DC, Nyasa DC, Songea MC, Songea DC na Tunduru DC.
Mipaka ya Kanda
Kwa upande wa Kusini Kanda imepakana nan chi ya Msumbiji; Kaskazini mikoa ya Morogoro na Pwani na Magharibi ni Nchi ya Malwai na Mikoa ya Iringa na Mbeya. Kwa upande wa Mashariki Kanda imepakana na Bahari ya Hindi.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15