NEMC YATUNUKU TUZO KWA TANTRADE UTUNZAJI WA MAZINGIRA MSIMU WA SABASABA


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetunuku tuzo ya heshima kwa Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu utunzaji wa Mazingira, katika hafla ya kufunga maonesho ya biashara kimataifaya 49 iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo

Akikabidhi tuzo hiyo, kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bi.Latifa Khamis, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi amesema NEMC imekabidhi tuzo hiyo kwa kutambua tano bora za utunzaji na usafi wa Mazingira uliosimamiwa nao katika kipindi chote cha Maonesho ya sabasaba 2025.

Dkt. Semesi amezianisha tano Bora hizo ambazo ni;

Ubunifu siku ya maalumu ya Mazingira ambayo iliadhimishwa tarehe 06.07.2025, mandhari ya maonesho kuwa safi na ya kupendeza kipindi chote cha Maonesho, kuhamasisha matumizi ya Nishati safi, kuhamasisha washiriki kutumia bidhaa ambazo ni rafiki kwa Mazingira na kufaulu kudhibiti taka licha ya idadi kubwa ya watu kutembelea maonesho hayo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali Wakuu wa Serikali akiwemo Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa ambaye ndiye mgeni rasmi na aliyefunga maonesho ya sabasaba 2025, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Seleman Jafo pamoja na Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali.

Maonesho ya biashara kimataifa kwa mwaka 2025 yamebeba Kaulimbiu mbiu isemayo "𝙈𝙖𝙤𝙣𝙚𝙨𝙝𝙤 𝙮𝙖 𝙗𝙞𝙖𝙨𝙝𝙖𝙧𝙖 𝙮𝙖 𝙆𝙞𝙢𝙖𝙩𝙖𝙞𝙛𝙖 𝙎𝙖𝙗𝙖𝙨𝙖𝙗𝙖, 𝙁𝙖𝙝𝙖𝙧𝙞 𝙮𝙖 𝙏𝙖𝙣𝙯𝙖𝙣𝙞𝙖".

Aidha, yamehudhuriwa na takribani nchi 22 na asilimia 70 ya wawekezaji wameweza kufikia malengo yao na kuongeza idadi ya wadau na masoko.

Baraza linaendelea kuhimiza wawekezaji na watanzania wote kwaujumlakuendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya utunzaji wa Mazingira kwa ajili ya Tanzania endelevu, safi na salama