KANDA YA ZIWA VIKTORIA MAGHARIBI

Utangulizi

NEMC Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi ni mojawapo ya kanda 13 za Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira. (NEMC) yenye jukumu la kusimamia na kutoa huduma katika Mikoa ya Geita, Kagera na Shinyanga.

Kanda hii ilianzishwa rasmi mwezi Novemba, 2025, kufuatia mgawanyo wa Kanda ya Ziwa Victoria kuwa kanda mbili, ambazo ni Ziwa Victoria Mashariki na Ziwa Victoria Magharibi, ili kuongeza ufanisi na kutoa  huduma kwa ukaribu. Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi inasimamia eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 86,104, likiwa ni eneo muhimu kwa shughuli za kiuchumi hususani uchimbaji na uchenjuji wa madini, uvuvi, kilimo na mazao ya misitu. 

Taswira ya Kanda Kimazingira

Eneo linalosimamiwa na Ofisi ya Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi lina jumla ya wakazi 8,208,206 kwa mujibu wa  Sensa ya Mwaka 2022. Kiujumla eneo hili limekuwa ni kivutio cha watu wengi kunakochangiwa kwa kiwango cha juu na shughuli za kiuchumi katika nyanda za kilimo, viwanda, ufugaji, uchimbaji na uchenjuaji madini, uvunaji wa mazao ya misitu, ujenzi wa nyumba za biashara na makazi. Wingi wa watu na shughuli hizo kumepelekea mabadiliko ya kiuchumi, kimazingira na kijamii kwa kiasi kikubwa. Aidha, Kanda ina maeneo ya vivutio vizuri kwa  watalii wa ndani na nje ya nchi kama vile Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha RubondoHifadhi ya Taifa ya Burigi–Chato, Hifadhi ya Taifa ya Ibanda–Kyerwa, Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika–Karagwe, , Pori la Akiba la Kigosi na Ziwa Victoria

Majukumu ya Kanda

Ofisi ya Kanda ya Ziwa Magharibi inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria  ya Mazingira Sura 191. Majukumu mahsusi ni pamoja na:

  • Mapitio ya Tathmini ya Athari  ya Mazingira kwa miradi ya maendeleo na uwekezaji
  • Kufanya ufuatiliaji juu ya Uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira
  • Kufanya tafiti za kimazingira
  • Kupokea na kufanya mapitio ya vibali vya taka hatarishi
  • Kukuza weledi juu ya masuala ya Mazingira
  • Kupokea na kutatua malalamiko ya kimazingira

Mawasiliano

Unaweza kufika au kuwasaliana na Ofisi kwa anuani ifuatayo:

Meneja wa Kanda,

NEMC – Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi,

Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,

Ghorofa ya 3,

Mtaa wa Magogo B,

 S.L.P. 253, Geita,

TANZANIA.

Simu: 0767153776

Barua pepe: nemc.geita@nemc.or.tz