Mradi unaohusika na kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya zebaki kwenye uchimbaji mdogo wa dhahabu nchini

Mmiliki wa Mradi: Benki ya Dunia
Wakala Mtendaji: (NEMC)
Mfadhili wa Mradi: Benki ya Dunia
Muda wa Utekelezaji: 2020 – 2025

Mradi huu ambao unajulikana kama Environmental Health and Pollution Management Project (EHPMP) ni mkakati mmojawapo wa utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa (National Action Plan-2020-2025) wa miaka 5 wa kutekeleza Mkataba wa Minamata ambao Tanzania imeridhia kuhusu kupunguza matumizi ya zebaki kwenye uchimbaji mdogo wa dhahabu. Mradi wa EHPMP unalenga kupunguza au ikiwezekana kuondosha kabisa matumizi ya zebaki kwenye uchimbaji ndogo wa madini ya dhahabu hapa nchini.

Mradi huu ni wa miaka 5 (2021-2025) ambao unafadhiliwa na Global Environment Facility (GEF) na msimamizi wa mradi huu ni Benki ya Dunia. Mradi huu ni sehemu ya mradi mkubwa unaotelekezwa kwenye Nchi 5 barani Afrika ambao unajulikana kama Africa Environmental Health and Pollution Management Program. Nchi hizo ni Kenya, Ghana, Zambia, Senegal na Tanzania.

Kwa Tanzania, mradi huu unatekelezwa kwenye mikoa 7 yenye kufahamika kuwa na wachimbaji wadogo wengi wa madini ya dhahabu. Mikoa hiyo ni Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Singida, Mbeya na Songwe. Mradi huu ulisainiwa tarehe 19/10/2020 kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania na ulitangazwa kuanza kutekelezwa rasmi manmo tarehe 26/10/2020. Hata hivyo, utekelezaji wa mradi ulichelewa kutokana na changamoto mbalimbali kama COVID 19 na kupelekea fedha kutoka Benki ya Dunia kuchelewa na mradi kuanza uekelezaji mwezi Octoba 2021.

Dhana halisi ya mradi huu ni kukabiliana na madhara ya kiafya na mazingira yatokanano na matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa madini aina ya dhahabu. Kama ambavyo inafahamika, zebaki ina madhara makubwa ya kiafya kwa binadamu lakini pia ina athari kwa mazingira. Madhara ya kiafya ni pamoja na magonjwa ya Minamata ambayo yanajumuisha kuathirika kwa Mfumo wa Neva na kusababisha magonjwa kama miguu na mikono kufa ganzi na kukosa nguvu, misuli kulegea, figo kuathirika, uono hafifu, kupoteza uwezo wa kusikia na kuongea, mimba kuharibika, kuzaa watoto taahira, kupoteza kumbukumbu, kukosa usingizi kwa muda mrefu, kiharusi na hatimaye kifo.

Mradi unatarajiwa kuteeleza yafuatayo:

  1. Kuimarisha wa mifumo ya kitaasisi, kujenga uwezo na maarifa kwa Taasisi mbalimbali katika kusimamia na kudhibiti athari zitokanazo wa matumizi ya Zebaki kwenye uzalishaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo.
  2. Kuwezesha Majadiliano ya Kisera na Kuimarisha Udhibiti (Support policy dialogue and regulatory enhancement). Hii kinaunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha na kusimamia Sera na Sheria za Mazingira kwa lengo la kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo ili kudhibiti athari za kiafya na kimazingira zitokanazo na matumizi ya zebaki kwenye uchimbaji mdogo wa dhahabu.
  3. Kuonesha Matumizi ya Teknolojia Mbadala (Demonstrating applications of Technology Approaches). Sehemu hii itagharimia utafiti wa teknolojia mbadala na kutengeneza vifaa vinavyohitajika ili kuondokana na matumizi ya zebaki.