Miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
MRADI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI WILAYANI KONGWA
Mtekelezaji wa Mradi: Foundation for Energy Climate and Environment (FECE) na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
Msimamizi wa Mradi Kitaifa: Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Bajeti ya mradi: US $ 1,200,000 ( Takribani TZS bil 2.7)
Muda wa mradi: Miaka 3
Wanufaika wa mradi: Wananchi Kata za Ugogoni na Mtanana
Malengo ya Mradi:
- Kusaidia upatikanaji wa maji ya uhakika kwa wakulima na wafugaji katika kata za Ugogoni na Mtanana (Kuwezesha shughuli za wananchi ziwe endelevu na ziweze kuhimili mabadiliko ya tabia ya nchi
- Kutunza mazingira ili yaweze kuwalinda wananchi dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi
- Kujenga uwezo wa tasisi na maofisa katika wilaya ya Kongwa juu ya namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza
Baadhi ya shughuli za mradi zitahusisha:
- Kuchimba visima vya maji
- Kujenga matanki ya kuhifadhi maji
- Kujenga mtandao wa kusambaza maji
- Kujenga malambo ya kunyweshea mifugo pamoja na kufufua majosho
- Kufufua makingamaji yaliyokuwepo tangu enzi za ukoloni ili kuhifadhi maji na kukuza kilimo endelevu
- Kupanda miti ya matunda na mbao, pamoja na mbegu bora ya nyasi za kulishia mifugo
- Kutoa elimu ya hifadhi ya mazingira na kuhuisha mipango ya Halmashauri ya Wilaya kuzingatia uhimili wa mabadiliko ya tabianchi
MRADI WA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIA YA NCHI ZANZIBAR
Mtekelezaji wa Mradi: Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Idara ya Mazingira
Msimamizi wa Mradi Kitaifa: Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Bajeti ya mradi: US $ 1,000,000 ( Karibia TZS bil 2.3)
Muda wa mradi: Miaka 3
Wanufaika wa mradi: Shehia ya Bubwini ( Wilaya ya Kaskazini B – Unguja) na Shehia ya Tovuni (Wilaya ya Wete- Pemba)
Malengo ya Mradi:
- Ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua ili kuwezesha upatikanaji wa maji muda wote
- Kuwezesha utekelezaji wa mbinu za kilimo hifadhi ili kutunza undogo, maji na kuongeza uzalishaji wa mazao
- Kusaidia shughuli mbalimbali rafiki kwa mazingira zenye kuingiza kipatao kwa wananchi ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi
- Kujenga uwezo wa tasisi na maofisa katika idara mbalimbali ngazi ya shehia, wilaya na taifa ili waweze kuweka mipango mahususi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuweza kusambaza tarifa na mambo ya kujifunza kutoka kwenye mradi.
MRADI WA UVUNAJI MAJI WA KIMKAKATI KUWEZESHA UHIMILI WA MABADILIKO YA TABIANCHI -DODOMA, SINGIDA NA TABORA
Mtekelezaji wa Mradi: Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine
Msimamizi wa Mradi Kitaifa: Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Bajeti ya mradi: US $ 1,280,000 ( Karibia TZS bil 2.9)
Muda wa mradi: Miaka 3
Wanufaika wa mradi: Wilaya ya Bahi, Manyoni, Igunga na Nzega
Malengo ya Mradi:
- Kujenga na kukarabati mabwawa ya kuvuna maji ili kuwezesha shughuli za kilimo, mifugo, pamoja na kuchimba visima vya maji kwa matumizi ya binadamu.
- Kuandaa na kutekeleza mpango shirikishi wa upandaji miti ya matunda, kuni, mbao na kuanzisha vitalu vya miti;
- Kuwezesha shughuli mbalimbali za kujiongeza kipato na ktk njia inayozingatia uhimili wa mabadiliko ya tabianchi kama vile upandaji miti, uanzishaji wa vitalu vya miti, ufugaji wa samaki, nk.
- Kuandaa na kutekeleza mbinu za kukabiliana na wadudu waharibifu na magonjwa ya mifugo na mimea yanayojitokeza kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi ili kuboresha uzalishaji wa kilimo na mifugo
MRADI WA KUKABILI MABADILIKO YA TABIANCHI BUNDA
Mtekelezaji wa Mradi: Halmashauri ya Wilaya ya Bunda
Msimamizi wa Mradi Kitaifa: Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Bajeti ya mradi: US $ 1,400,000 ( Karibia TZS bil 3.2)
Muda wa mradi: Miaka 3
Wanufaika wa mradi: Kata za Iramba, Neruma, Namhura, Kitengule, Nyahihoro na Igundu Wilayani Bunda
Malengo ya Mradi:
- Kukarabati miundombinu ya maji na kupanua wigo wa mtandao maji vijijini;
- Kuchimba visima vya maji kwa maeneo yasiyo karibu na vyanzo;
- Kuwezesha shughuli mbadala za kuinua vipato vya wananchi kama vile kutengeneza miundimbinu ya kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa samaki, kuku, nyuki nk
- Kupanda miti ya matunda, mbao na kuni na kuhifadhi mifumoikolojia iliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi
- Kutoa elimu ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya
TULIPO SASA
Miradi miwili wa Kongwa na SWAHAT imezinduliwa na kuanza utekelezaji rasmi. Mradi wa Zanzibar uko tayari kuzinduliwa wakati wowote mwezi huu au mapema Disemba. Mradi wa Bunda uko kwenye hatua ya usajili kwenye mfumo wa wizara ya fedha wa kusajili miradi ya fedha za nje. Baada ya usajli utazinduliwa na kuanza utekelezaji…labda mwishoni mwa Disemba