​WAZIRI JAFO AZUNGUMZIA USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA COP28


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi COP28, uliofanyika kuanzia 30/11/2013- 12/12/2023 Dubai UAE.

Katika Mkutano huo Tanzania itanufaika zaidi na fedha za miradi, teknolojia, utaalam na Programu mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo Programu ya Afrika ya Nishati Safi ya Kupikia; programu ya Afya na mabadiliko ya tabianchi; na utekelezaji wa Mikakati ya kuimarisha uhimili katika katika sekta ya Maji, Misitu na Bahari. Aidha, wafanya biashara na wawekezaji wa Tanzania wamekutana na wawekezaji kutoka nje ya nchi na kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji kwenye eneo la mabadiliko ya tabianchi ambapo jumla ya taasisi na kampuni zaidi ya 56 zimeonesha nia ya kuwekeza nchini kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Aidha Mhe. Jafo amewafahamisha waandishi wa habari kuwa

Mkutano wa 29 (COP29) umepangwa kufanyika Azerbaijan 11-22 Novemba 2024, na Mkutano wa 30 (COP30) utafanyika nchini Brazil tarehe 10-21 Novemba 2025