WAZIRI JAFO AHAMASISHA WANAFUNZI KUPANDA MITI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara ya kuhamasisha wanafunzi na wanajamii kupanda miti katika Shule ya SekondariKaribuni iliyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam mapema Leo machi 25, 2022.

Akizungumza katika ziara hiyo ambayo inalenga kuhamasisha upandaji Miti katika Shule za msingi na Sekondari katika kampeni ya "SOMA NA MTI", Mhe. Jafo amesema kampeni hiyo inalenga hasa kuchagiza ajenda ya maendeleo yaupandaji miti na uhifadhi wa mazingirana kuwafanya wanafunzi kuwa na utamaduni wa kupanda miti kuanzia wakiwa wadogolengo ikiwa ni kuifanya Tanzania ya kijanina kuyahifadhi mazingira yetu.

Aidha, Waziri Dkt. Jafo ameongeza kuwa kampeni ya "SOMA NA MTI" inaonesha dhamira ya kuwaelekeza wanafunzi wawe mstari wa mbele katika upandaji Miti " Hakika hii inaonesha dhamira yetu ni kuwaelekeza wanafunzi wawe nao mstari wa mbele na ni dhamira Yetu kusababisha agenda hii iwe ni miongoni mwa agenda wanafunzi wanaishi nayo. Leo hii tunashuhudia miti inakatwa hovyo hata minazi, mifenesi, miembe na mikorosho ambayo mababu zetu waliipandaleo hii watu wanaikata na kuuza magogo ni kwa sababu suala zima la elimu ya mazingira liko chini, Imani yangu kubwaendapo swala hili litapandikizwa kwa wanafunzi Taifa letu litafika maeneo ambapo suala la mazingira litakuwa ni jambo muhimu sana".

Kampeni ya SOMANA MTI ambayo tayari ilishazinduliwa katika wilaya ya Ubungo na Sasa katika wilaya ya Temeke inalenga kupanda miti elfu sabini na moja (71,000) kwa upande wa Shule za Sekondari pekee na kwa upande wa Shule za msingi takribani miti isiyopungua laki Moja na elfu tisini (190,000) inatarajiwa kupandwa na kwa ujumla itakuwamiti zaidi ya laki mbili na elfu sitini ( 260,000) na uhakika wa upatikanaji wa miti hiyo kutoka wakala wahuduma za misituTanzania ( Tanzania Forest Services Agencies TFS), ambapo kuna vitalu vya miti zaidi ya laki Tano ( 500,000) kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam pekee.

Waziri Dkt Jafo amehitimisha Kwa kuwaasa watanzania kutunza mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

"Tukumbuke hivi karibuni nchi yetu ilianza kupitia katika kiangazi kikubwa sana takribani katika miezi minane (8), tulishuhudia katika mikoa mbalimbali wanyama wakifa , maji kukaukana hata katika mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya mikoa mingine Tanzania hali ni mbaya sana.