TANZANIA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI (COP 27).
TANZANIA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI (COP 27).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe.Dkt.Selemani Jafo amesema kuwa Tanzania itashiriki katika mkutano wa wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika tarehe 7-8 Novemba 2022 Sharm El- Sheikh nchini Misri.
Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe takribani 35000 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo wakuu wa Nchi na serikali, Mawaziri na wataalamu waliobobea katika masuala ya mabaliko ya tabianchi.
Waziri Jafo amethibitisha ushiriki wa Tanzania katika mkutano na kuongeza kuwa Tanzania imedhamiria kushiriki kitofauti na miaka ya nyuma katika mikutano iliyopita kwa kuandaa banda la maonesho ambalo litakuwa na shughuli na maonesho ya kazi za kuitangaza Nchi ya Tanzania.
Aidha Dkt.Jafo amesema Tanzania itashiriki kikamilifu katika majadiliano ya masuala yenye maslahi mapana kwa Nchi yetu na kuweka msimamo katika uhimilivu wa mabadiliko ya Tabiachi, upunguzaji gesi joto na masoko ya kaboni na mbinu zisizo za masoko ili kukabiliana au kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi ili kutangaza utalii wa Tanzania na kuhifadhi mazingira yetu.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15