​RC. NJOMBE APONGEZA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI MKUU NEMC


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka kwa utendaji wake mzuri wa kazi hasa kwenye masuala ya Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake.

Amesema kwa uwajibikaji wake huo umesaidia kupunguza malalamiko mengi yahusuyo mazingira na utekelezaji wa miradi hali iliyowezesha uwekezaji kukua kwa kiwango kusudiwa katika Nchi yetu.

"Nampongeza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Gwamaka kwa namna ambavyo ameisimamia Taasisi kwa kupunguza malalamiko mengi hasa kwa kuanzisha Ofisi za Kanda ambazo sasa zimepunguza gharama kwa wadau kupata huduma, lakini pia tunampongeza kwa kuendelea kutoa elimu kabla ya adhabu katika masuala ya Mazingira" Amesema Mhe. Mtaka.

Ameongeza kuwa kwa NEMC kuanzisha ofisi za Kanda Nchi nzima ni uzalendo wenye tija kwani imesogeza huduma kwa wadau hali iliyopelekea kupunguza gharama kwa wawekezaji katika upatikanaji wa huduma