NEMC yateketeza zaidi ya mifuko mbadala milioni 2 iyochini ya kiwango Mwanza
BARAZA la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeteketeza Zaidi ya mifuko mbadala milioni mbili iliyotengenezwa chini ya kiwango na kiwanda cha Jin Yuan Investment kilichopo Jijini Mwanza na gunia nane ya vifungashio viliyoingizwa nchini kwa njia za magendo.
Akizungumza mara baada ya kufanya zoezi la uteketezaji wa mifuko hiyo jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt.Samuel Gwamaka alisema zoezi hilo liwe onyo kwa wazalishaji wengine ambao hawafuati utaratibu na kanuni za viwango zilivyoweka za 70 gsm ili kulinda soko la ndani la bidhaa hizo. “Lengo letu ni kulinda viwanda vya ndani ili vipande masoko ya bidhaa wanazozalisha lakini imekuwa ni kinyume kwa wawekezaji kuzalisha mifuko iliyochini ya kiwango cha gsm 70 ambayo imepitishwa na Shirika la Viwango nchini(TBS),” alisema Dkt.Gwamaka. Alisema kuwa hali hiyo inachangia udhibiti wa mifuko inayotoka nje ya nchi kuwa mgumu, hivyo Baraza kuanziasha ukaguzi nchi nzima kwa lengo la kubaini wazalishaji wa ndani wasiofuata taratibu na kuwachukulia hatua ikiwemo kuteketeza bidhaa na kuwapiga faini. “Wazalishaji wakifuata sheria na viwango vilivyowekwa vya 70 gsm na uweka nembo ya mzalishaji kwenye mifuko inayozalishwa nchini itasaidia kubaini mifuko iliyochini ya kiwango na kufanya wepesi kwa mamlaka kushukua hatua,” alisema Dkt.Gwamaka
Aliongezea kuwa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli ni kujenga uchumi wa kati na viwanda hivyo NEMC ipo katika kutekelza azma hiyo kwa kushirikiana na wawekezaji kwa kutoa elimu na miongozo mbalimbali juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira. “Niwaombe wafanyabiashara kuacha kuingiza mifuko mbadala kutoka nje ya nchi iliyochini ya kiwango kwa kufanya hivyo wanakuwa wanahujumu uchumi wa nchi pamoja na wawekezaji wa ndani kwa kuleta bidhaa zilizochini ya kiwango,” alisema Dkt.Gwamaka alisema NEMC itaendelea na ukaguzi ili kuhakikisha bidhaa za mifuko mbadala inayozalishwa nchini inafuata sheria na viwango vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na kuweka nembo na anwani ya mzalishaji, uzito unaoweza kubebwa na mfuko huo. Alitoa rai kwa wananchi kuachana na matumizi ya mifuko isiyo na nembo ya mzalishaji kwani inapeleka kuua soko la mifuko mbadala inayozalishwa nchini na kwa kufanya hivyo watakuwa wanashiriki katika uhujumu uchumi inakuendelea kutumia ifuko hiyo ntoa taarifa kwa
wazalishaji wanaokwenda kinyume cha sheria.
Aidha, Baraza limewataka wazalishaji wote walipigwa faini kwa kosa la kuzalisha mifuko iliyochini ya kiwango kuzilipa faini hizo ndani ya muda uliowekwa pamoja na kuteketeza kwa moto bidhaa au kuzirejeleza na kufanya uzalushaji unaofuata viwango na kanuni zilizowekwa. Kwa Upande Mjumbe wa Bodi ya NEMC, Bw.Damas Masologo amesema Baraza lipo katika kutekeleza sheria za nchi katika kutunza mazingira na sio kuvifungia viwanda tutaendelea kutaendelea kutoa elimu kwa wawekezaji nchini ili waendane na kanuni na sheria za nchi. “Tunashukuru uongozi wa kiwanda cha Nyakato Steel Mills kwa kutoa nafasi katika kiwanda chake ili kuteketeza mifuko hiyo pasipo kuathiri mazingira katika zoezi la uteketezaji,” alisema Bw.Masologo NEMC itaendelea kushirikiana na Serikali za Mkoa, Wilaya na taasisi nyingine za kiserikali katika kuhakikisha wazalishaji wa mifuko mbadala nchini wanafata kanuni na viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) ili kujenga soko la /bidhaa za ndani nchini.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15