NEMC YATEKETEZA TANI 44.4 ZA VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI VISIVYOKIDHI VIWANGO


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) leo limeteketeza tani 44.4 za vifungashio vya Plastiki visivyokidhi viwango.

Akizungumza katika zoezi hilo la uteketezaji Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Samwel Gwamaka amesema vifungashio hivi ni vile visivyopaswa kuingia sokoni kwani havikidhi vigezo stahiki vilivyowekwa na Serikali kwa ajili ya matumizi hayo.

" Leo tuko hapa, tunateketeza vifungashio Tani 44.4, hivi vifungashio havipaswi kuingia sokoni na ndio maana tunachukua jukumu la kuviteketeza Ili kuwaonesha wengine kwamba havipaswi kuwa kwenye Mazingira kwa sababu vikiingia huathiri ustawi wa jamii." Amesema Gwamaka.

Ameongeza kuwa ni vema umma wa watanzania ukaelewa umuhimu wa zoezi hili na kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha linatekelezeka kwa ufanisi na kiwango kilichokusudiwaha Twiga Cement Jijini Dar es Salaam.