NEMC YASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA MKOANI KIGOMA.


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika. Maonyesho hayo yanafanyika mkoani Kigoma katika uwanja wa BOT uliopo karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Akiongea katika maonyesho hayo Meneja wa NEMC Kanda ya Magharibi Benjamin Dot to amesema kuwa NEMC imeshiriki katika maonyesho hayo ili kuweza kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusiana na utunzaji na Uhifadhi wa mazingira pamoja na usajili wa miradi, ulipaji wa ada na tozo na tathimini ya athari kwa mazingira na mambo mengine mbalimbali.

"Maonyesho haya ni muhimu yatasaidia sisi Baraza kutoa elimu kuhusiana na utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa wananchi wanaoshiriki katika maonyesho haya ambayo yanajumuisha Nchi zote zinazozunguka Ziwa Tanganyika yani Tanzania, Rwanda, Burundi, Zambia na Congo DRC." alisema Bwana Dotto

Naye Afsa Mazingira kutoka NEMC Kanda ya Mashariki Bi Edith Makungu amesisitiza wananchi washiriki katika maonyesho hayo pamoja na kutilia maanani suala zima la ulipaji wa ada na tozo za mazingira ambalo mwisho wa malipo hayo ni tarehe 30 juni mwaka huu.

"Tunawasisitiza na kuwakumbushawale wote ambao hawajalipa tozo na ada za mazingira kujitahidi kulipa ndani ya muda kwani kulipa ada na tozo za mazingira ni muhimu kwa mustakabali wa mendeleo ya Taifa letu" alisema