NEMC Yapongezwa


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais, Mazingira na Muungano Mh. George Simbachawene, amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia kanuni na sheria iliyopo na amelitaka baraza kuendelea kusimamia sheria na kanuni zake ilikuweza kufanya kazi kwa uadililifu na kutenda haki kwa kila mtu. Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na menejiment ya NEMC baada ya kuwasili ofisi za NEMC zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Aidha Mhe. waziri ameonyesha kuwa na matumaini makubwa na Baraza katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa na mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kusimamia mazingira Nchini.

Mkurugenzi Mkuu Dkt. Gwamaka ametoa pongenzi kwa waziri simbachawene na kutoa shukrani za dhati kwa kutembelea ofisi za NEMC baada ya kuteuliwa hivi karibuni, na kuahidi kuwa Baraza litatoa ushirikiano wa dhati ili kutekeleza na kufanikisha vizuri majukumu yake na dhamana aliyopewa na mhe. Rais.