MFUKO WA DUNIA WA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI (ADAPTATION FUND) UMEPITISHA MIRADI MIWILI ITAKAYO RATIBIWA NA NEMC YENYE THAMANI YA KIASI CHA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 2.2


Mfuko wa dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabia ya nchi (Adaptation Fund) kupitia kwa Bodi ya taasisi hiyo (Adaptation Fund Board) umepitisha miradi miwili kati ya minne iliyowasilishwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 2.2.

Miradi hiyo ambayo ni, “Kukabili Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Jamii ya Wafugaji na Wakulima Wilaya ya Kongwa na ‘‘Kukabili Mabadiliko ya Tabia ya nchi katika jamii za Pwani ya Zanzibar” yote ikiwa na lengo la kutatua changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo hayo.

Miradi hii miwili nchini itaratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamamizi Wa Mazingira (NEMC) na kutekelezwa na taasisi zilizoshinda miradi hiyo (Excuting Entities) ambazo kwa mradi wa Kongwa ni Foundation For Energy, Climate and Environment (FECE) inayoshirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na mradi wa Zanzibar ni Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Baraza linasubiri majibu ya miradi miwili iliyobaki kati ya minne iliyowasilishwa kwa taasisi hiyo.

Aidha kupitishwa kwa miradi hiyo ni mafanikio makubwa kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na kuwa mratibu wa mfuko huo hapa nchini.