NEMC YASHIRIKI MKUTANO WA MABORESHO YA MFUMO WA UKUSANYAJI TAKA NGUMU.


Baraza laTaifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeshiriki mkutano wa pamoja na Mataifa Mbalimbali kutoka Barani Afrika na kituo cha Sayansi na Mazingira cha India wenye lengo la kuboresha mfumo wa ukusanyaji taka ngumu kwenye Miji na Majiji.

Mkutano huo uliofanyika Posta jijini Dar es salaam umelenga pia kujadili namna bora ya kuongeza mnyororo wa thamani kweye taka zinazozalishwa ambapo kwa kufanya hivyo taka nyngi zitarejezwa na kiasi kinachobaki kitahifadhiwa kwa namna ambayo ni rafiki wa mazingira.